ELCT North Eastern Diocese
Ziara ya kikazi ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, Jimbo la Kusini
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 20/01/2022 amekuwa na ziara ya kikazi katika Jimbo la Kusini na ameongoza kikao kazi kilicho jumuisha Wachungaji, Mashemasi pamoja na wainjilisti wa KKKT-DKMs Jimbo la Kusini pamoja na mambo mengine yaliyo jadiliwa katika kikao hicho kilichofanyika katika Usharika wa soni Baba Askofu amewakumbusha watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa uwazi na umakini mkubwa katika kila jambo wanalo lifanya.
- Hits: 14150
Ibada ya mazishi ya Mchungaji mstaafu Anthony Danga Mndeme
- Details


Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 19/01/2022 ameongoza Ibada ya mazishi ya Mchungaji mstaafu Anthony Danga Mndeme katika Usharika wa Mamba jimbo la Kusini.
- Hits: 19906
Ibada ya mazishi ya Mama Damaris Appelesy Ketto
- Details

Askofu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,leo tarehe 18/01/2022 ameongoza Ibada ya mazishi ya marehemu Mama. Damaris Appelesy Ketto,mama mzazi wa Mkuu wa Jimbo la Pwani, Mch Thadeus A. Ketto ,

Ibada hiyo imefanyika katika Usharika wa Mtonga jimbo la tambarare.marehemu Mama. Damaris Appelesy Ketto aliitwa mbinguni jioni tarehe 14/01/2022. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.



- Hits: 13816
Pumzika kwa amani Mama, DAMARIS APPELESY KETTO
- Details

Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio,wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza , yamekwisha kupita UFUNUO 21:4.
Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Mama. Damaris Appelesy Ketto,mama mzazi wa Mkuu wa Jimbo la Pwani, Mch Thadeus A. Ketto ,kilichotokea jana Ijumaa tarehe 14/01/2022.Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Jumanne tarehe 18/01/2022 katika Kanisa la KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Usharika wa Mtonga - Korogwe. Uongozi unatoa pole kwa Mkuu wa Jimbo la Pwani, Mch. Thadeus A. Ketto, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe
- Hits: 14781
Page 91 of 137

