ELCT North Eastern Diocese
Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu afanyamazungumzo na Mch. P. Butiku toka Sinodi rafiki ya Southeastern Pennsylvania Synod
- Details

Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 28/12/2021 amepata nafasi ya kufanya mazungumzo na Mch. P. Butiku toka Sinodi rafiki ya Southeastern Pennsylvania Synod, USA akileta Salam rasmi kutoka kwa Askofu Patricia Davenport Mkuu wa Sinodi hiyo. Katika ujumbe wa salam za Askofu Davenport alikaza umuhimu wa kuimarisha uhusiano na urafiki.
- Hits: 14365
siku ya baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Mlalo Jimbo la Kaskazini
- Details
Leo tarehe 26/12/2021 Imekuwa siku ya baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Mlalo Jimbo la Kaskazini ambapo kijana mmoja alipata kipaimara na Watoto 29 walibatizwa, Liturgia katika Ibada hiyo iliongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs Mch. Michael Mlondakweli Kanju.
- Hits: 14099
Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch.Dkt Msafiri Joseph Mbilu leo Tarehe 25/12/2021 ameongoza Ibada katika Kanisa Kuu (Cathedral) Lushoto.Ikiwa leo ni sikukuu ya Krismas Baba Askofu Mbilu amehubiri neno la Mungu kutoka kitabu cha Luka 2:10 nalo linasema “Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote”.
- Hits: 14894
Page 93 of 137


