ELCT North Eastern Diocese
Pumzika kwa amani Mzee Tamilwai Agustino Baruti
- Details

TANZIA
"Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita " UFUNUO 21:4.
Kaimu Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya Uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Baba Mzazi wa Mch. Lemmy Baruti, Mzee Tamilwai Augustino Baruti kilichotokea usiku wa tarehe 31/10/2021 katika hospitali ya Wilaya ya Pangani.
Taratibu za mazishi zinaendelea na mtajulishwa.
Uongozi unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.

........... ................ ................. .....................
- Hits: 15235
Ibada ya Kipaimara KKKT-DKMs,Usharika wa Irente
- Details

Leo tarehe 31/10/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Irente Jimbo la Kusini ambapo vijana wapatao 24 walipata kipaimara.
- Hits: 15800
IBADA YA KIPAIMARA KKKT-DKMs, Usharika wa Hale.
- Details

Leo tarehe 30/10/2021 Imekuwa siku ya baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Hale Jimbo la Tambarare kwani vijana wapatao 164 walipata kipaimara na sita 6 kati yao walibatizwa.
- Hits: 15711
Maadhimisho miaka 60 ya Kwaya Kuu Lushoto
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mch Dkt. Alex Malasusa amewakumbusha waimbaji kuwa uimbaji unamchango mkukwa katika kumuita mtu kwa mungu na uimbaji umetumika kama chombo cha uinjilisti hivyo kukuwa kwa injili katika KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na sehemu nyingine upo mchango mkubwa wa waimbaji.

- Hits: 16190
Page 100 of 137

