ELCT North Eastern Diocese
Toggle Navigation
  • Home
  • Our Diocese
  • Wopa
  • Gallery
  • Institutions
    • Irente Children's Home
    • Irente School for the Blind
    • Rainbow School
    • Lwandai Secondary School
    • Lutindi Mental Hospital
    • Bangala Lutheran Junior Seminary
    • Bumbuli Hospital
    • SEKOMU university
    • Namna ya kuchangia kazi za maendeleo na Vituo vya kutoa huduma kwa watu wenye mahitaji maalumu (KKKT-DKMs)
  • Calendar
  • Projects
    • Irente Biodiversity Reserve
    • UTC - Usambara Technological Center
    • Restaurants and Hostels
      • Tumaini Mbuyukenda Hostel and Restaurant
      • Martin Luther Garden and Restaurant
      • Tumaini Songe Restaurant and Hostel
      • Hohen Restaurant and Hostel
      • Tumaini Lushoto Restaurant and Hostel
  • Superintendent
    • Coast Superintendent
    • Northern Superintendent
    • Southern Superintendent
    • Plains Superintendent
  • New-clips
  • Contact us
  • You are here:  
  • Home

Bishop Rev.Dr. Msafiri J. Mbilu

Change Language

English German Spanish Swahili Swedish

News & Updates

  • TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI YA KAZI Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya...
  • Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji  NSSF

    Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF

    Leo tarehe 01/04/2026, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amepokea ugeni kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifa...
  • TAARIFA

    TAARIFA

    Uongozi wa KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ukiwakilishwa na Katibu Mkuu Mwl. Julius Madiga, u...
  • ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Dkt. Msafiri Jos...
  • Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Dayosisi yetu imepata heshima kubwa ya kushiriki katika Mkutano wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na U...

.



 

 

Staff Email

ELCT North Eastern Diocese

Ibada ya Kipaimara Usharika wa Mshihwi , Youths Confirmation at Mshihwi Lutheran Parish

  • Print
Details
Published: 27 November 2021

 

Leo tarehe 27/11/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Mshihwi kanda ya Magoma, Jimbo la Tambarare, ambapo vijana wapatao 63 walipata kipaimara. 

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu. Ibada ilihudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti, Mashemasi, Kwaya, Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Mshihwi. 

Katika risala ya vijana hao waliopata kipaimara wamemshukuru Baba Askofu Dkt. Mbilu kwa kutenga muda wake na kushiriki katika Ibada hiyo, kipekee wameushukuru uongozi wa KKKT-DKMs pamoja na watenda kazi wengine wa KKKT-DKMs kwa namna wanavyo fanya kazi kubwa ya kuirejesha Dayosisi katika hadhi yake ya awali.

Katika siku hii vijana hao wanapothibitisha imani yao ya Kikristo waliyobatizwa nayo walipo kuwa watoto wadogo wameungana na uongozi wa Dayosisi katika kuunga mkono masuala ya elimu kwa kuchangia jumla ya Tsh.189,000.

Awali Baba Askofu aliyeambatana na msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs, Mch. Michael Mlondakweli Kanju walipata nafasi ya kufungua nyumba ya mtumishi katika Usharika huo wa Mshihwi kanda ya Magoma.

Hits: 13915

Ibada ya Kipaimara Usharika wa Mshihwi , Youths Confirmation at Mshihwi Lutheran Parish

  • Print
Details
Published: 27 November 2021
Hits: 13747

Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu, awashukuru wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

  • Print
Details
Published: 26 November 2021

Mnamo tarehe 26/11/2020 Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alichaguliwa kuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Askofu Dkt. Mbilu alichaguliwa kuwa Askofu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki baada ya kufanyika Mkutano Mkuu wa 3  baada ya miaka 125 ya Injili ulioanza tarehe 25-26/11/2020 mkutano uliokuwa na ajenda kuu moja ya Uchaguzi wa Askofu  mpya wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na viongozi wengine.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati maalumu ya kuratibu shughuli za mkutano mkuu wa uchaguzi alikuwa Askofu Mstaafu Dkt. Paulo Akyoo toka KKKT Dayosisi ya Meru ambaye baada ya uchaguzi alimtangaza Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu aliye chaguliwa na Wajumbe wa mkutano Mkuu kuwa Askofu mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kupata kura 194  sawa na 89.4% .

Askofu Mteule alimteua Mch Michael Mlondakweli Kanju ambaye alithibitishwa na mkutano Mkuu kwa kura ya Siri na kufanikiwa kupata kura 170 Kati ya 210 sawa na 80.9%. Kura hizo ni zaidi ya 2/3 ambalo ni hitaji la kikatiba. Aidha Mkutano Mkuu ulichaguwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki baada ya kupatikana kwa Halmashauri kuu hiyo ilitimiza wajibu wake wa Kikatiba wa kuchaguwa  Wakuu wa Majimbo na kuwaleta mbele ya Mkutano mkuu.

Ikiwa tayari umetimia mwaka mmoja leo tarehe 26/11/2021 Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu anawashukuru wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa ushirikiano mzuri waliouonesha kwa kuunga mkono kazi mbalimbali zinatotekelezwa katika Dayosisi.

Shukrani hizo amezitoa alipokuwa anafanya mahojiano maalumu na kituo cha redio cha Utume Fm pamoja na kitengo cha Habari na mawasiliano cha KKKT-DKMs.

Askofu   Dkt. Mbilu ambaye alizaliwa tarehe 9 Mei, 1968 katika kijiji cha Kwang’wenda, Soni, Wilayani  Lushoto Mkoa wa Tanga, alianza kukalia kiti hicho cha uaskofu tarehe 09/05/2021, siku ambayo aliingizwa kazini.

Askofu Dkt. Mbilu  alibarikiwa kuwa Mchungaji Februari 19, 1995, alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Kwang’wenda, Lushoto. Mwaka 1985-1988 alipata elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Namfua iliyopo wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro. Alipata elimu ya Theologia, Chuo cha Theologia, Makumira mwaka 1990- 1994 na kumaliza masomo ya General Certificate in Theology.

Mwaka 1997 alijiunga na masomo ya shahada ya Theolojia chuo kikuu cha Makumira na kuhitimu mwaka 2000. Alipata shahada ya uzamili ya Theolojia mwaka 2000-2002 huko Norway, katika chuo cha Stavanger School of Mission and Theology.

Mwaka 2006-2012 alijiunga na chuo kikuu cha Kirchliche Hochschule Wuppertal cha nchini Ujerumani ambapo alitunukiwa shahada ya uzamivu katika Theolojia. Kabla ya kufikia nafasi hiyo amewahi kuwa Mwalimu Chuo cha Biblia Vuga 1994-1997 na pia amewahi kuwa Mchungaji Kiongozi Usharika wa Mombo, mwaka 1997-1999 na Usharika wa Korogwe 2003.

Aliwahi pia kuwa Mkuu wa Jimbo la Kaskazini na Mchungaji wa Usharika wa Mlalo kuanzia mwaka 2004 hadi 2006, na mwaka 2012 alikuwa Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kange. Askofu  Dkt. Mbilu amewahi kuwa Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira 2012- 2015.

Pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa kituo cha Tanga cha Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastiani Kolowa, (SEKOMU) mwaka 2015-2016. Vilevile alikuwa Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho kati ya mwaka 2016 hadi 2018 na mhadhiri chuoni hapo katika masomo ya Agano Jipya na Lugha za Biblia (Kigiriki).

Hadi siku anachaguliwa kuwa Askofu Mteule, Askofu Dkt. Mbilu alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika chuo kikuu cha Silliman, akifundisha masomo ya Agano Jipya na Lugha za Biblia (Greek na Hebrew).

NDOA

Alifunga ndoa na Mary Joseph Jali Desemba 9, 1995 na wamejaliwa kupata watoto watatu, Sarah Mbilu, Joseph Mbilu na Jackskon Mbilu.

WAKUU WA MAJIMBO

Pia Halmashauri Kuu ya Dayosisi, iliwachagua Mch. Frank Mntangi kuwa Mkuu wa Jimbo la Tambarare, Mch. Issai Amasia Mweta kuwa Mkuu wa Jimbo la Kusini, Mch. Anderson Kipande kuwa Mkuu wa Jimbo la Kaskazini na Mch. Thadeus A. Ketto Mkuu wa Jimbo la Pwani. Wakuu hawa wa majimbo walitangazwa  wazi na kupokelewa rasmi katika Mkutano Mkuu wa Dayosisi uliofanyika Kanisa Kuu Lushoto (Cathedral) tarehe 25-27/11/2020.

Hits: 15173

Ukawe sehemu ya watakao rithi uzima wa milele

  • Print
Details
Published: 26 November 2021

Mwanamke mwema ni taji la mumewe ;bali aaibishae ni kama kuoza mifupani mwake. Mithali 12: 4 haya yamehubiriwa leo tarehe 26/11/2021 na Mchungaji Sabina Lumwe katika ibada ya ufunguzi wa warsha ya wake wa wachungaji na mashemasi kutoka Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Dayosisi ya Mashariki na Pwani. ambapo Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ndiye aliyekua mgeni rasmi wa warsha hiyo inayofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa SEKOMU-Lushoto Tanga

Askofu Dkt Msafiri Mbilu wakati wa ufunguzi amesoma neno kutoka kitabu cha Mithali 12:2 na kusisitiza wake wa Wachungaji waendelee kuwa taji kwa kufanya mema na kumcha Mungu sambamba na hilo amewasisitizia kutokujichanganya kwengine bali kukumbuka wao kuwa ni Walutheli.

Hata hivyo baba Askofu amesisitiza  utanashati, upole, uaminifu na kutopenda utajiri wa haraka haraka ni vitu muhimu kwa mke wa Mchungaji, mbali na hayo mke wa Mchungaji anapaswa kuwa mchakarikaji na kuwa mpambanaji kwenye suala zima la kuimarisha kipato cha familia.

Warsha hii imeandaliwa na UEM kwa kushirikiana na Dayosisi ya Kaskazini Mashariki pamoja na Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

UEM: United Evangelical Mission ni chama Cha kiinjili Cha kimisioni kilichoanzishwa miaka 25 iliyopita na wamisionari kutoka Ujerumani wa Rhenish na Betheli ambao walifika Africa, na Asia kwa ajili ya kuanzisha shughuli za Dini. Katika Africa walifika katika nchi 7 ambazo ni Tanzania, DR Congo, Africa ya Kusini, Botswana, Cameroon, Namibia na Rwanda kukiwa na madhehebu 15. Katika Tanzania inawakilishwa na Makanisa 4 ya KKKT ambayo ni KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na KKKT Dayosisi ya Karagwe.

Aidha Chama hiki kinashughulika katika nguzo tano ambazo ni Uhusiano/ Undugu, Diakonia, Uinjilishaji, Utetezi pamoja na Maendeleo.

Hits: 15376
  1. Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, kufungua warsha ya wake wa wachugaji na mashemasi
  2. Majibu juu ya zilipo fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya Dayosisi kupatikana.
  3. Ibada ya Kipaimara Usharika wa Mgwashi Jimbo la Kusini
  4. Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs, Mch Michael Mlondakweli Kanju afungua Kongamano la Maombi na Maombezi

Page 97 of 137

  • 92
  • 93
  • 94
  • ...
  • 96
  • 97
  • 98
  • 99
  • ...
  • 101

Back to Top

© 2026 ELCT North Eastern Diocese