
Leo tarehe 31/10/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Irente Jimbo la Kusini ambapo vijana wapatao 24 walipata kipaimara.

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu. Ibada ilihudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti,Mashemasi,Kwaya,Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Irente.

Katika risala ya cijana hao waliopata kipaimara kipekee wamemshukuru msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs Mch. Michael Mlondakweli Kanju pamoja na kaimu Katibu Mkuu wa KKKT-DKMs Mch Godfrey Tahona Walalaze pamoja na watenda kazi wengine wa KKKT-DKMs kwa namna wanavyo fanya kazi kubwa ya kuirejesha Dayosisi katika hadhi yake ya awali.

Vijana hao wamemtia moyo Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu kwa neno la Mungu kutoka kitabu cha Ezr 10:4, Yos 1:9 “Inuka maana shuhuli hii yakuhusu wewe na sisi tu pamoja nawe uwe na moyo mkuu ukaitende. Je si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; Usiogope wala usifadhaike kwa kuwa Bwana Mungu wako yu pamoja nawe kila uendako.





