ELCT North Eastern Diocese
ASKOFU DKT. FREDRICK ONAEL SHOO KUFANYA ZIARA KKKT-DKMs
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema kuwa hana mashaka na kazi inayoendelea ya ujenzi wa Kanisa jipya katika Usharika wa Mombo kutokana na kasi na mwenendo mzuri wa ujenzi wa Kanisa hilo.
- Hits: 14596
Salamu za Pasaka za Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu
- Details

“Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka” (Marko 16:6).
Wapendwa katika Bwana, kufufuka kwa Yesu ni tendo la matumaini kwa ajili ya maisha mapya. Wanawake waliokuwa jasiri walipoingia ndani ya kaburi walistaajabu kukuta kaburi tupu, ndipo wakapewa ujumbe huu kuwa msistaajabu Yesu mnayemtafuta amefufuka. Waliondoka kaburini wakiwa na hofu kuu huku wakibeba ujumbe huu wa kufufuka kwa Yesu.

Tendo hili la kufufuka kwa Yesu linadhihirisha maisha mapya ng’ambo ya kaburi. Kwa kufufuka kwa Yesu tunauona ukuu na nguvu ya Mungu ikitudhihirishia kuwa kaburi siyo mwisho wa matumaini yetu.

Dunia tunayoishi imejaa majanga makubwa na hofu nyingi. Katika mwaka huu tunasikia majanga ya vita iliyosababishwa na uvamizi wa Taifa la Urusi kuivamia Ukraine. Vita hivi vimeleta madhara mengi kwa dunia tunayoishi mfano kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa mbalimbali muhimu, vifo kwa watu wasio na hatia kama vile Watoto, Kinamama, wagonjwa mahospitalini, kuharibika kwa miundo mbinu ya muhimu na mengine mengi ya kutisha. Haya yote yanaleta simanzi mioyoni mwa walio wengi.

Lakini ujumbe wa kufufuka kwa Yesu unaamsha maisha mapya na kuleta furaha mpya kuwa hata katikati ya giza nene bado lipo tumaini kuu. Yesu aliyesulibiwa sasa yu hai na anatupa tumaini la uhai kwetu sisi sote tunaomwamini. Kaburi kwetu si kitu cha kutisha tena kwakuwa yeye tunayemwamini ameshinda nguvu za kabaru na kuzimu.

Tuungane na wanawake hawa jasiri kuubeba ujumbe wa kufufuka kwa Yesui ili uwafikie watu wote duniani.

- Hits: 14890
Balozi Fanuel Kuzilwa azikwa nyumbani kwao Mlalo
- Details

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Ufunuo 14:13

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 16/04/2022 akiwa katika Usharika wa Mlalo Jimbo la Kaskazini ameongoza Ibada ya mazishi ya Balozi Fanuel Ismail Kuzilwa.


Balozi Fanuel Kuzilwa aliyezaliwa tarehe 21/07/1945 ameitwa mbinguni tarehe 12/04/2022, akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

KATIKA UTUMISHI: Marehemu Balozi Kuzilwa katika uhai wake aliwahi kushika nafasi mbalimbali za kiuongozi, aliwahi kuwa Afisa Mwandamizi- Ubalozi wa Tanzania Nchini Angola na Nigeria.KATIKA TEUZI ZA RAIS aliteuliwa kuwa – Mkurugenzi wa Idara ya Africa, Wizara ya Mambo ya nje,Mnikulu, Balozi.Hata hivyo uongozi wa KKKT-DKMs utaendelea kumkumbuka Marehemu Balozi Kuzilwa kwa juhudi zake katika kuhakikisha Chuo Kikuu cha SEKOMU kinafunguliwa.

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, unatoa pole kwa Familia ya Marehemu Balozi Fanuel Kuzilwa, ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu mzito. Mungu awape nguvu na faraja ya kweli katika kipindi hiki kigumu. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.


- Hits: 16266
Ibada ya Mazishi ya Mzee Nicholas Mkala
- Details
Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio,wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza , yamekwisha kupita UFUNUO 21:4.

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju leo tarehe 14/04/2022 ameongoza Ibada ya mazishi ya Marehemu Mzee Nicholas Fredrick Mkala ambaye pia ni kaka wa Mch. Lewis Fredrick Shemkala wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Usharika wa Hale.

Ibada imefanyika katika Kitongoji cha Kwamongo,Kijiji cha Kihitu,Kata ya Vuga Jimbo la Bumbuli,Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Marehemu Mzee Nicholas Fredrick Mkala aliitwa mbinguni Jumatatu ya tarehe 11/04/2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa anapatiwa matibabu.

Kwa niaba ya Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,kupitia kwa msaidizi wa Askofu Mch. Michael Kanju ambaye alimuwakilisha Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Mch Dkt Msafiri Mbilu kwenye Ibada hiyo ya mazishi amesema kuwa, Uongozi unatoa pole kwa Familia ya Marehemu, ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huo mzito. Mungu awape nguvu na faraja ya kweli katika kipindi hiki kigumu. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.






- Hits: 13918
Page 85 of 137

