ELCT North Eastern Diocese
Askofu Dkt. Msafiri Mbilu aahidi kuboresha Maslahi kwa Wainjilisti
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameahidi kusimamia Maslahi na kuboresha hali ya kiutumishi kwa kila Mwinjilisti aliyeajiriwa na Dayosisi ikiwemo kuwekewa michango katika mfuko wa hifadhi ya jamii na kwamba hakuna Mwinjilisti atakae staafu bila ofisi ya Askofu kujua.

Askofu Dkt. Mbilu ameeleza hayo leo tarehe 09/06/2022 wakati akifungua semina ya siku nne iliyoandaliwa kwa Wainjilisti wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki yenye lengo la kuwajengea uwezo,inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benjamin Mkapa SEKOMU.
- Hits: 16409
Mch. Geoffrey Mwakihaba awekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa awamu ya Tano KKKT-Dayosisi ya Konde
- Details

KATIKA PICHA: Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa awamu ya Tano KKKT-Dayosisi ya Konde Mch. Geoffrey S. Mwakihaba, Ibada hiyo imefanyika leo tarehe 05/06/2022, katika Usharika wa Kanisa Kuu tukuyu-Mbeya


na kuongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluther Tanzania (KKKT) Askofu Dkt.Fredrick Shoo huku Liturgia ikiongozwa na Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch.Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.


...............................

Hapo jana katika Ibada maalumu ya kuwekwa wakfu vifaa vya kiuaskofu iliyo ongozwa na Askofu Mstaafu wa Dayosisi hiyo Askofu Dkt. Israel Peter Mwakyolile katika Usharika wa Kanisa Kuu tukuyu Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch.Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ndiye aliye hubiri katika Ibada hiyo.

- Hits: 15243
Pumzika kwa amani Bibi,Hilgati A. Kika
- Details

Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.

Leo tarehe 30/05/2022 imefanyika Ibada ya mazishi ya Marehemu Bibi,Hilgati A. Kika katika Usharika wa Makorora Jimbo la Pwani. Marehemu Bibi,Hilgati Kika katika uhai wake alikuwa muimbaji wa kwaya Kuu KKKT-DKMs Usharika wa Makorora.

Marehemu Bibi,Hilgati ambaye pia ni mama mdogo wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, mwili wake umepumzishwa katika makaburi ya Bombo area Jijini Tanga.


Marehemu Bibi Hilgati alizaliwa tarehe 01/07/1948 katika Kijiji cha Kwang’wenda Wilayani Lushoto aliitwa mbinguni alfajiri ya tarehe 28/05/2022 katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga- Bombo.

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unaendelea kutoa pole kwa,familia ya marehemu,Kwaya Kuu Makorora, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.


- Hits: 13169
Askofu Dkt. Mbilu -Tuendelee kupunguza deni la Dayosisi
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameendelea kuwa kumbusha Washarika wa Usharika wa Kange na Dayosisi kwa ujumla kuendela kuchangia Deni la Dayosisi na kusema kuwa taarifa ya michango hiyo itaendelea kutolewa kama ilivyo fanyika awali.

amewakumbusha Washarika hao leo tarehe 29/05/2022 ni siku ya Bwana kabla ya Pentekoste, SIKU YA CCT Neno Kuu (Sikia Kuomba kwetu) Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameongoza Ibada ya Jumapili katika Jimbo la Pwani Usharika wa Kange na kuwasihi Washarika na Wanadayosisi kuona umuhimu wa kutoa sadaka ya CCT.
- Hits: 15249
Page 81 of 137

