ELCT North Eastern Diocese
Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo afungua semina elekezi kwa wasaidizi wa Maaskofu
- Details

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dkt. Fredrick Shoo leo tarehe 14/06/2022 amefungua semina elekezi kwa wasaidizi wa maaskofu inayofanyika makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Iringa.Maaskofu wapatao 27 wa Dayosisi za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wanahudhuria semina hiyo ya siku nne juu ya kazi za Mission na Uinjilishaji kwenye mazingira ya sasa yeye utandawazi na upotoshaji wa mafundisho sahihi ya neno la Mungu ndani ya Kanisa.
- Hits: 12609
Ibada ya Jumapili na Harambee ya ujenzi wa Kanisa
- Details

leo tarehe 12/06/2022 Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju ameongoza Ibada ya Jumapili na harambee ya ujenzi wa Kanisa la Mtaa wa Sakura ambao ni senta ya Usharika Mteule wa Ng'ambo ya Mto Pangani.
- Hits: 17507
Askofu Dkt. Msafiri Mbilu awapongeza Wainjilisti wa KKKT-DKMs
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema kuwa Wainjilisti ni jeshi kubwa katika Dayosisi, linalofanya kazi kubwa na nzuri inayoonekana kwa kuwafikia wana Dayosisi kwa ukaribu zaidi.

Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 12/06/2022 kwenye Ibada ya Jumapili na kilele cha juma la Uinjilisti katika Dayosisi ambapo Wainjilisiti wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki wapatao 211 wameshiriki kwenye Ibada hiyo iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto.

Hata hivyo Askofu Dkt. Mbilu hakusita kuwajulisha Wainjilisti na Wanadayosisi kwa ujumla juu ya ujio wa Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) ambacho kipombioni kukamilisha usajili wake ili kuanza udahili katika mwaka huu wa masomo wa 2022/2023.


Ikumbukwe kuwa Askofu Dkt. Mbilu alipata wasaa wa takribani siku nne ya kukaa na Wainjilisti wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwenye semina iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo Wainjilisti hao hasa katika nyakati hizi zilizo jaa mafundisho potofu ya neno la Mungu semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benjamin Mkapa SEKOMU ambapo pia Baba Askofu Dkt Msafiri Mbilu alipata nafasi ya kuwasikiliza Wainjilisti hao juu ya changamoto wanazo zipata na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi.



- Hits: 15614
Habari Picha semina ya Wainjilisti
- Details

KATIKA PICHA: Semina ya Wainjilisti wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Askofu iliyokuwa inafanyika katika ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa (SEKOMU) ambapo leo tarehe 11/06/2022 semina hiyo imefungwa rasmi na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, hapo kesho Wainjilisti hao wanatazamiwa kushiriki Ibada ya Jumapili Kanisa Kuu Lushoto.
- Hits: 13816
Page 80 of 137

