ELCT North Eastern Diocese
TANZIA
- Details

Kaimu katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Bi. Catherine Mlondakweli Kanju ambaye ni mama mzazi wa msaidizi wa Askofu Mch.Michael Mlondakweli Kanju,kilichotokea leo Alhamisi tarehe 22/07/2021 katika kituo cha afya cha St Joseph Kwamndolwa Korogwe Tanga alikokuwa anapatiwa matibabu.Mazishi yatafanyika siku ya Jumatatu tarehe 26/07/2021 Saa sita mchana nyumbani kwao Lutindi.Uongozi unatoa pole kwa Baba Dean Mch. Michael Mlondakweli Kanju, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
- Hits: 15852
Hitimisho la Ziara ya Maaskofu toka Ethiopian Evangelical Church Mekane Yesus - Ethiopia
- Details

Rais wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani LWF Askofu Dkt. Pant Filibus Musa (KUSHOTO) akiwa na Askofu Dkt.Msafiri Joseph Mbilu wa KKKT- DKMs
RAIS wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani LWF, ASKOFU Dkt Panti Musa amesema kuwa umoja ulioyakutanisha Makanisa ya Kiinjili ya Kilutheri Tanzania na Kanisa la Kilutheri la Ethiopia Mekane Yesus unapaswa pia kuwa katika ngazi za Sharika katika Nchi hizo na siyo kwa ngazi ya viongozi ili uwe alama ya matumaini kwenye ulimwengu wa sasa.
- Hits: 16245
Ibada ya Kipaimara KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Usharika wa Makorora.
- Details

Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki leo tarehe 11/07/2021 ameongoza Ibada ya Jumapili iliyokuwa na tendo la kuwabariki vijana wa kipaimara katika Usharika wa Makorora Jimbo la Pwani. Liturgia iliongozwa na Mkuu wa Jimbo la Pwani Mch Thadeus A. Ketto.
- Hits: 20725
Page 108 of 137


