ELCT North Eastern Diocese
Ufunguzi wa Kanisa Usharika wa Msongolo Mtaa wa Sinai, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
- Details

Tarehe 26/06/2021 imekuwa siku ya furaha katika Dayosisi yetu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ambapo katika Jimbo la Kusini tumekuwa na Ufunguzi wa Kanisa katika Usharika wa Msongolo mtaa wa Sinai.Katika ufunguzi huo Ibada iliongozwa na Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu .
- Hits: 17075
Ziara ya Mch Michael Mlondakweli Kanju KKKT Dayosisi ya Karagwe
- Details

Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki , Mch Michael Mlondakweli Kanju yupo ziarani KKKT Dayosisi ya Karagwe ambapo leo tarehe 25/06/2021 ameongoza ibada ya kufunga mwezi wa sita katika Kanisa Kuu la Lukajange .Akihubiri katika ibada hiyo kutoka kitabu cha Ufunuo wa Yohana 21:4 amesema kuwa kuna mahangaiko ya aina mbalimbali, machozi ya kila namna,maumivu pamoja na magonjwa,na hali ngumu ya maisha. Hii ni hali ya maisha ambayo watu wanapitia. Bwana Yesu anaahidi kwamba atafuta machozi haya na hayatakuwepo tena.
- Hits: 17441
Mwendelezo wa ziara ya Mch Yared A. Wakami KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
- Details

Msaidizi wa Askofu kutoka KKKT Dayosisi ya Karagwe, Mch Yared A. Wakami ameipongeza KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki hususani wafanya kazi wa vituo vya Irente Rainbow School,Irente School for the Blind,Irente Farm pamoja na kituo cha Irente Children’s Home kwa namna wanavyo tumika kwa uaminifa katika kuvitunza vituo hivyo.
- Hits: 16383
Ziara ya Mch Yared A. Wakami KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
- Details

Msaidizi wa Askofu toka KKKT Dayosisi ya Karagwe , Mch Yared A. Wakami yupo ziarani KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambapo leo tarehe 14/06/2021 ametembelea ofisi za wakuu wa majimbo ya Pwani na Tambarare.
- Hits: 16702
Page 110 of 137

