ELCT North Eastern Diocese
Nafasi za masomo Seminari ndogo ya Bangala
- Details

Uongozi wa Shule ya Seminari ndogo ya Bangala iliyopo Halmashauri ya Bumbuli Vuga inawatangazia nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2022 kwa vijana waliomaliza darasa la saba mwaka huu 2021, mtihani wa kujiunga utafanyika tarehe 11/09/2021 na tarehe 25/09/2021. fomu za kujiunga zinapatikana katika vituo vifuatavyo.
Shuleni Bangala,Tumaini Bookshoop(Lushoto),Korogwe , Muheza, Handeni, Makorora, Kana.Pia tuna nafasi chache za wanaopenda kuhamia katika shule yetu kwa kidato cha tatu.
- Hits: 17085
Ziara ya kikazi Shule ya Sekondari Lwandai
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 30/08/2021 amefanya ziara ya kikazi katika Shule ya Sekondari Lwandai. Katika ziara hiyo Baba Askofu Mbilu alitembelea mazingira ya Shule na kupokea taarifa iliyowasilishwa na Mkuu wa Shule hiyo, Mch. Daniel Mwarabu na waandamizi wa idara mbalimbali za shule hiyo.
- Hits: 15163
JUBILEE YA MIAKA 30 YA WACHUNGAJI WANAWAKE 1991-2021
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewapongeza wachunguji walio barikiwa mnamo tarehe 30,06,1991 na kuingia katika hudumu ya kichungaji tayari kutumika shambani mwa Bwana.
- Hits: 18737
Ziara ya Mch.Dkt.Ulrich Mouller KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch.Dkt.Msafiri Joseph Mbilu amekutana na kufanya mazungumzo na Mch.Dkt.Ulrich Mouller (Vice moderator UEM) ambaye aliambatana na Mch.Dkt. Ernest Kadiva (The deputy Executive secretary in Africa) Leo tarehe 14/08/2021 alipo tembelea makao makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

- Hits: 14808
Page 105 of 137

