ELCT North Eastern Diocese
Toggle Navigation
  • Home
  • Our Diocese
  • Wopa
  • Gallery
  • Institutions
    • Irente Children's Home
    • Irente School for the Blind
    • Rainbow School
    • Lwandai Secondary School
    • Lutindi Mental Hospital
    • Bangala Lutheran Junior Seminary
    • Bumbuli Hospital
    • SEKOMU university
    • Namna ya kuchangia kazi za maendeleo na Vituo vya kutoa huduma kwa watu wenye mahitaji maalumu (KKKT-DKMs)
  • Calendar
  • Projects
    • Irente Biodiversity Reserve
    • UTC - Usambara Technological Center
    • Restaurants and Hostels
      • Tumaini Mbuyukenda Hostel and Restaurant
      • Martin Luther Garden and Restaurant
      • Tumaini Songe Restaurant and Hostel
      • Hohen Restaurant and Hostel
      • Tumaini Lushoto Restaurant and Hostel
  • Superintendent
    • Coast Superintendent
    • Northern Superintendent
    • Southern Superintendent
    • Plains Superintendent
  • New-clips
  • Contact us
  • You are here:  
  • Home

Bishop Rev.Dr. Msafiri J. Mbilu

Change Language

English German Spanish Swahili Swedish

News & Updates

  • TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI YA KAZI Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya...
  • Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji  NSSF

    Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF

    Leo tarehe 01/04/2026, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amepokea ugeni kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifa...
  • TAARIFA

    TAARIFA

    Uongozi wa KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ukiwakilishwa na Katibu Mkuu Mwl. Julius Madiga, u...
  • ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Dkt. Msafiri Jos...
  • Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Dayosisi yetu imepata heshima kubwa ya kushiriki katika Mkutano wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na U...

.



 

 

Staff Email

ELCT North Eastern Diocese

Mkuu wa KKKT aanza ziara yake KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

  • Print
Details
Published: 27 July 2022

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Fredrick Shoo leo tarehe 27/7/2022 ameanza ziara rasmi ya kuitembelea KKKT–Dayosisi ya Kaskazini Mashariki itakayoambatana na kufungua na kuweka mawe ya msingi na kuongea na wana Dayosisi katika maeneo mbalimbali.


Akiwasili katika eneo la Bwiko Usharika Mteule wa Mkumbara Askofu Dkt. Shoo amepokelewa na mwenyeji wake Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu na wana Dayosisi na baadae aliwasili katika Usharika wa Mombo ambapo ameweka jiwe la msingi la Kanisa jipya na kuongoza Ibada ya Shukrani.


Akihubiri neno la Mungu katika Ibada hiyo kutoka kitabu cha Injili ya Mathayo 7:1-5 Mkuu wa Kanisa amekemea tabia za baadhi ya Wakristo kujihesabia haki na kuhukumu wengine hatua inayofifisha vipawa na karama za wengi katika kulijenga Kanisa la Mungu.


Mkuu wa Kanisa amesema kwakuwa hakuna mtu aliyekamilika kabisa hivyo waliowakristo waonyane kwa upendo bila kunyosheana vidole madhaifu ya wengine.


Mbali na hayo Mkuu wa Kanisa ameendesha harambee kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kanisa la Usharika huo wa Mombo na kuchangia kiasi cha shilingi 1,000,000.


Nae Askofu wa KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Mbilu amewapongeza wanadayosisi kwa namna walivyojitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mkuu wa KKKT na kuwasihi kuendelea kujitokeza katika maeneo yote ya Majimbo ambapo Mkuu wa Kanisa atatembelea.


Kesho tarehe 28/07/2022 msafara wa Mkuu wa KKKT utaelekea Bumbuli, ambapo Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo ataendelea na ziara yake katika Jimbo la Kusini kwa kutembelea Usharika wa Bumbuli, Hospitali ya Bumbuli, Chuo cha Utabibu Bumbuli (BUCOHAs) na kisha ataelekea Lutindi ambapo atapata wasaa wa kuwasalimu Washarika wa Lutindi na kutembelea Hospitali ya wagonjwa wa akili Lutindi (Lutindi Mental Hospital).

 

 

Hits: 13705

Matukio katika picha Ibada ya Jumapili.Jimbo la Kaskazini Usharika wa Mbaramo

  • Print
Details
Published: 24 July 2022

MATUKIO KATIKA PICHA: Ibada ya Jumapili iliyokuwa na matukio mbalimbali ikiwemo Ufunguzi wa nyumba ya mwinjilisti pamoja na Ibada ya kipaimara katika Usharika wa Mbaramo ambapo vijana wapatao 85 wamebarikiwa huku mmoja kati yao akibatizwa.Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ndiye aliyeongoza Ibada hiyo.

 

 

Hits: 11897

Askofu Dkt. Mbilu ahimiza elimu juu ya uanzishwaji wa miradi kwa vijana.

  • Print
Details
Published: 23 July 2022

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema kuwa elimu kwa vijana juu ya uandaaji na usimamizi wa miradi ni vema sasa ikatolewa katika Dayosisi nzima ili kuwa na vijana wenye uelewa wa kuandaa miradi mbalimbali itakayo wakwamua kiuchumi na kuisaidia jamii.

Askofu Dkt.Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 23/07/2022 akiwa katika Usharika wa Muheza kwenye kilele cha mafunzo ya  muda mfupi ya uandaaji wa miradi,Tathimini Shirikishi ya Mafunzo (Participatory Learning Appraisal) pamoja na Upangaji wa mradi wenye muelekeo wa matokeo (Result Oriented Project ) yaliyoanza tarehe 11/07/2022 hadi tarehe 23/07/2022 yakijumuisha  vijana wapatao 16  wa Usharika huo.

Nimefurahi kwa Usharika,Washarika,Kamati ya miradi  kuwawezesha vijana hawa kupata mafunzo haya hasa kwenda vijijini kuona matatizo yalipo katika jamii kuandika miradi kwa wafadhili itakayo wapatia fedha zitakazo isaidia jamii, HILI NI JAMBO ZURI NALA KUPONGEZA. Alisema Askofu Mbilu.

Awali katika Ibada ya Jumuiya iliyo jumuisha jumuiya zote za Usharika huo iliyo ongozwa na Baba Askofu Dkt, Mbilu katika Usharika huo, amemshukuru Mkuu wa Jimbo la Tambarare Mch. Frank Mtangi, Mchungaji wa Usharika wa Muheza Mch. John Ndimbo wakufunzi pamoja na kamati mbalimbali zilizowezesha kufanikisha mafunzo hayo kwa vijana na kutoa wito kwa Majimbo na Sharika zingine kuiga jambo hilo.

Hits: 12335

Ziara ya Mkuu wa KKKT katika Dayosisi yetu

  • Print
Details
Published: 22 July 2022

Wapendwa  wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki yahusu ziara rasmi ya kikazi ya Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Baba Askofu Dkt. Fredrick O. Shoo katika Dayosisi yetu kuanzia tarehe 27/07/2022 hadi tarehe 02/08/2022.

 Dhumuni la ziara ya Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo ni kuitembelea KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, kufungua na kuweka mawe ya msingi. Vilevile Baba Askofu Dkt. Shoo atapata wasaa wa kuongea na wana Dayosisi katika maeneo mbalimbali.

 Baba Askofu atawasili katika Dayosisi yetu tarehe 27/07/2022 siku ya jumatano saa 4:00 asubuhi, punde atakapokanyaga ardhi ya Mkoa wa Tanga katika eneo la Bwiko atapokelewa na mwenyeji wake Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu na wana Dayosisi. Ataanza ziara yake siku hiyohiyo ya tarehe 27/07/2022 katika Jimbo la Tambarare kwa kuweka jiwe la msingi la Kanisa jipya katika Usharika wa Mombo muda saa 6:00 mchana.

 Aidha mara baada ya uwekwaji wa jiwe la msingi msafara wa Mkuu wa KKKT utaelekea katika Jimbo la Kusini ambapo Baba Askofu Dkt. Shoo ataongea na wana Dayosisi katika Usharika wa Soni yalipo Makao Makuu ya Jimbo hilo majira ya saa 10:00 jioni. Mara baada ya kuongea na wanadayosisi katika Usharika wa Soni siku hiyohiyo msafara utaelekea Kanisa Kuu Lushoto ambapo Mkuu wa KKKT atapokelewa rasmi kwa Ibada maalum saa 11:45 jioni.

 Tarehe 28/07/2022 msafara wa Mkuu wa KKKT utaelekea Bumbuli kuanzia saa 2:00 – 6:00 mchana, ambapo Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo ataendelea na ziara yake katika Jimbo la Kusini kwa kutembelea Usharika wa Bumbuli, Hospitali ya Bumbuli na Chuo cha Utabibu Bumbuli (BUCOHAs).

Majira ya saa 7:30 mchana hadi saa 12:00 jioni msafara wa Mkuu wa KKKT utaelekea Lutindi ambapo Baba Askofu atapata wasaa wa kuwasalimu washarika wa Lutindi na kutembelea Hospitali ya wagonjwa wa akili Lutindi (Lutindi Mental Hospital).

 Siku ya tarehe 29/07/2022 msafara wa Mkuu wa KKKT muda wa saa 3:00 hadi 6:00 mchana  utaelekea katika Jimbo la Tambarare ambapo itafanyika Ibada katika Usharika wa Korogwe na majira ya saa 7:00 mchana msafara utaelekea Jimbo la Pwani.

 Tarehe 30/07/2022 saa 3:00 – 6:00 mchana Baba Askofu ataweka jiwe la Msingi wa Kanisa la Makorora na kuongoza Ibada ya kipaimara katika Usharika huo wa Makorora.

 Tarehe 31/07/2022 Mkuu wa Kanisa ataongoza Ibada ya jumapili Kanisa Kuu Lushoto kuanzia saa 2:00 – 5:00 asubuhi na majira ya saa 8:00 – 10:00 jioni atatembelea vituo vya Irente Rainbow School, Irente Children’s Home, Irente School for the Blind na Irente Farm.

 Tarehe 01/08/2022 saa 4:00 – 5:00 asubuhi msafara wa Mkuu wa Kanisa utaelekea katika Jimbo la Kaskazini ambapo pia kutafanyika Ibada katika Usharika wa Mlalo na majira ya saa 6:30 -8:00 mchana ataelekea katika Shule ya Sekondari Lwandai ambapo Baba Askofu Dkt. Shoo atafungua tena Jengo la Maabara ambalo lilifanyiwa ukarabati  na majira ya saa 9:00 – 11:00 jioni msafara wa Mkuu wa Kanisa utaelekea katika Chuo  kitarajiwa cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI).

 Wito kutoka kwa Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu kwa wana KKKT – DKMs, ni kujitokeza kwa wingi kumpokea Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo sehemu zote atakazopita kuanzia Bwiko, Soni, Lushoto, Mlalo, Bumbuli, Lutindi, Tanga, Korogwe na maeneo yote yaliyotajwa atakapokuwa anatembelea, anafungua, anaweka mawe ya msingi na atakapokuwa anaongea nasi.

 Mwisho kama ilivyo kawaida na desturi ya wana KKKT-DKMs wakati tunapotembelewa na wageni hasa ugeni mkubwa wa Mkuu wetu wa KKKT, Baba Askofu Dkt. Fredrick O. Shoo, natoa wito tena kwenu kujitokeza kwa wingi tumpokee Mkuu wetu wa Kanisa katika Dayosisi yetu.

 

Hits: 13191
  1. IBADA YA KIPAIMARA KKKT-DKMs, Jimbo la Kaskazini,Usharika wa Mlalo.
  2. Katika picha Ibada ya Jumapili Usharika wa Ngwelo “B” Bumbuli,
  3. Happy Saba Saba Day!
  4. Askofu Mbilu awashukuru wana KKKT-DKMs

Page 77 of 137

  • 72
  • 73
  • 74
  • ...
  • 76
  • 77
  • 78
  • 79
  • ...
  • 81

Back to Top

© 2026 ELCT North Eastern Diocese