ELCT North Eastern Diocese
IBADA YA KIPAIMARA KKKT-DKMs, Jimbo la Kaskazini,Usharika wa Mlalo.
- Details

Leo tarehe 17/07/2022 imekuwa siku ya baraka tele kwa washarika wa Jimbo la Kaskazini ,Usharika wa Mlalo kwani vijana wapatao 116 walipata kipaimara na wanne 4 kati yao walibatizwa.

Katika Ibada hiyo Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ndiye aliye ongoza Ibada hiyo, huku Liturgia ikiongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs Mch. Michael Mlondakweli Kanju.


Katika Risala ya vijana hao waliobarikiwa iliyosomwa mbele ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu vijana hao wametambua jitihada za Baba Askofu pamoja na wasaidizi wake katika kusimamia mambo ya Elimu na Afya. Hata katika kipindi hiki ambacho Dayosisi inakabiliana na deni bado wameona na kushuhudia kazi za maendeleo zikiendelea kufanyika.

Wameeleza kujisikia fahari kuona shule za Dayosisi (Lwandai na Bangala) zikiboreshwa na kuvutia wanafunzi wengi zaidi. Huku wakitambua jitihada za kukifufua kilichokuwa Chuo cha SEKOMU,kwa hatua za awali za kuanzishwa kwa Chuo cha Kati cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kitakachotoa kozi ya famasia.







- Hits: 13134
Katika picha Ibada ya Jumapili Usharika wa Ngwelo “B” Bumbuli,
- Details

KATIKA PICHA: Ibada ya Jumapili kutoka Jimbo la Kusini Usharika wa Ngwelo “B” Bumbuli, ambapo Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ndiye aliyeongoza Ibada hiyo leo tarehe 10/07/2022.




Msaidizi wa Askofu Mch. Michael Mlondakweli Kanju

Mkuu wa Jimbo la Kusini Mch. Issai Mweta


- Hits: 12673
Happy Saba Saba Day!
- Details

Happy Saba Saba Day! Tanzania census August 2022 prepare to be counted
- Hits: 14521
Askofu Mbilu awashukuru wana KKKT-DKMs
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru wanadayosisi na wote walioshiriki katika maombi ya kumuombea mwenzi wake Mwl. Mary Mbilu katika kipindi chote cha kuugua kwake.
Ametoa shukrani hizo katika Ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kumponya na kumvusha katika kipindi kigumu cha kuugua kwa mwenzi wake na kusema kuwa maombi na sala za wanadayosisi ndugu jamaa na marafiki yamekuwa faraja kwao na kuwaomba kuendelea kuikumbuka familia hiyo katika maombi.
Katika hatua nyingine Askofu Dkt. Mbilu amewahimiza waumini na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika zoezi la sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyia mwezi Agosti,2022 kwa lengo la kupata takwimu sahihi kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla huku ikiongozwa na kauli mbiu isemayo: SENSA KWA MAENDELEO, JIANDAE KUHESABIWA


Aidha kwa upande wake Mwl. Christopher Mwakasege ambaye ndiye aliyehubiri neno la Mungu katika Ibada hiyo maalumu ya Shukrani iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto, amewataka waumini kujijengea tabia ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayowatendea kwani kwakufanya hivyo wanampa nafasi Mungu kuzidi kutenda miujiza juu yao.

Ibada hiyo ya Shukrani pia imehudhuriwa na Askofu Mstaafu wa KKKT-DKMs Mzee Joseph Jali,viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Kalisti Lazaro,Diwani wa Lushoto Mjini,Mkurugenizi wa Halmalmashauri ya Lushoto pamoja na ndugu jamaa na marafiki kutoka ndani na nje ya Dayosisi.




- Hits: 12873
Page 78 of 137

