ELCT North Eastern Diocese
Bodi ya Taasisi ya Elimu KOTETI yazinduliwa rasmi kuendelea na majukumu yake.
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amezindua rasmi Bodi ya Taasisi ya Elimu ya KOTETI chini ya mwenyekiti Profesa Joseph Kuzilwa,leo tarehe 8/02/2023.

Profesa Joseph Kuzilwa (Aliyesimama)
Sambamba na uzinduzi huo Askofu Dkt. Mbilu ameitaka Bodi hiyo kuifanya Taasisi ya Elimu ya KOTETI kuwa kituo chenye ubora, kuwa wabunifu na uthubutu wa kufanya mambo makubwa na kuhakikisha hakutokei anguko lolote kama ilivyokua kwa kilichokuwa Chuo Kikuu cha SEKOMU anguko lililopelekea Dayosisi kuingia kwenye madeni makubwa.


- Hits: 16076
Nafasi ya kazi Afisa Ustawi wa Jamii
- Details

UTANGULIZI
Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni miongoni mwa Dayosisi 27 ndani ya KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-DKMs ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi ifuatayo
- Afisa Ustawi wa Jamii
- Hits: 13339
Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs afungua kikao cha wadau wa kutengeneza mtaala wa Diakonia
- Details
Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju amefungua kikao cha wadau wa kutengeneza mtaala wa Diakonia, Ustawi wa Jamii na Speech ideology kilichofanyika katika ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopa katika chuo cha Kolowa Technical Training Institute ( KOTETI) Magamba leo tarehe 3/02/2023.
Mtaala huu unategemewa kuwa moja wapo ya kozi zitakazo tolewa katika taasisi ya Elimu KOTETI. Mch. Kanju aliongeza kuwa Dayosisi imebobea katika kutoa huduma za kijamii za Kidiakonia kwa kuwa na vituo vingi ambavyo vinawafikia watu wenye mahitaji maalum.
- Hits: 11840
Page 60 of 137


