
UTANGULIZI
Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni miongoni mwa Dayosisi 27 ndani ya KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-DKMs ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi ifuatayo
- Afisa Ustawi wa Jamii
MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI.
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe na umri usiopungua miaka 30 na usiozidi miaka 45.
- Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato Cha Nne, kidato cha Sita na Taaluma aliyosomea.
- Elimu kiwango cha kuanzia shahada moja ya Ustawi wa Jamii au shahada ya Maendeleo ya Jamii kutoka vyuo vinavotambulika
- Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili
- Awe na uzoefu wa kubuni na kuandika miradi pamoja na usimamizi pamoja na tathmini.
- Awe radhi kufanya kazi kwenye mazingira ya aina zote
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
MAOMBI YOTE YAAMBATANISHWE NA,
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
- Nakala ya cheti cha kidato cha nne au/ na cha sita au stashahada kulingana na kada ya mwombaji. Kwa aliyesoma nje ya nchi au mitaala ya nje ya nchi waambatanishe cheti cha ithibati kutoka baraza la mitihani Tanzania (NECTA).
- Maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V ).
- Picha ndogo (passport size) moja ya hivi karibuni.
- Nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA/ Namba ya NIDA).
- Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja na cheti cha kuzaliwa na NIDA hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa viapo na kusajiliwa na Msajili wa hati, wizara ya Ardhi na maendeleo ya makazi.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.
Maombi yote yatumwe ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili (mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 28/02/2023 ).
Maombi yote yatumwe kwa Ofisi ya Katibu Mkuu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
S.L.P 10 LUSHOTO
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

