Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amezindua rasmi Bodi ya Taasisi ya Elimu ya KOTETI chini ya mwenyekiti Profesa Joseph Kuzilwa,leo tarehe 8/02/2023.
  
Profesa Joseph Kuzilwa (Aliyesimama)
Sambamba na uzinduzi huo Askofu Dkt. Mbilu ameitaka Bodi hiyo kuifanya Taasisi ya Elimu ya KOTETI kuwa kituo chenye ubora, kuwa wabunifu na uthubutu wa kufanya mambo makubwa na kuhakikisha hakutokei anguko lolote kama ilivyokua kwa kilichokuwa Chuo Kikuu cha SEKOMU anguko lililopelekea Dayosisi kuingia kwenye madeni makubwa.