ELCT North Eastern Diocese
Toggle Navigation
  • Home
  • Our Diocese
  • Wopa
  • Gallery
  • Institutions
    • Irente Children's Home
    • Irente School for the Blind
    • Rainbow School
    • Lwandai Secondary School
    • Lutindi Mental Hospital
    • Bangala Lutheran Junior Seminary
    • Bumbuli Hospital
    • SEKOMU university
    • Namna ya kuchangia kazi za maendeleo na Vituo vya kutoa huduma kwa watu wenye mahitaji maalumu (KKKT-DKMs)
  • Calendar
  • Projects
    • Irente Biodiversity Reserve
    • UTC - Usambara Technological Center
    • Restaurants and Hostels
      • Tumaini Mbuyukenda Hostel and Restaurant
      • Martin Luther Garden and Restaurant
      • Tumaini Songe Restaurant and Hostel
      • Hohen Restaurant and Hostel
      • Tumaini Lushoto Restaurant and Hostel
  • Superintendent
    • Coast Superintendent
    • Northern Superintendent
    • Southern Superintendent
    • Plains Superintendent
  • New-clips
  • Contact us
  • You are here:  
  • Home

Bishop Rev.Dr. Msafiri J. Mbilu

Change Language

English German Spanish Swahili Swedish

News & Updates

  • TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI YA KAZI Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya...
  • Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji  NSSF

    Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF

    Leo tarehe 01/04/2026, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amepokea ugeni kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifa...
  • TAARIFA

    TAARIFA

    Uongozi wa KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ukiwakilishwa na Katibu Mkuu Mwl. Julius Madiga, u...
  • ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Dkt. Msafiri Jos...
  • Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Dayosisi yetu imepata heshima kubwa ya kushiriki katika Mkutano wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na U...

.



 

 

Staff Email

ELCT North Eastern Diocese

Ufunguzi wa kikao cha tathmini ya kazi za Dayosisi kwa mwaka 2022.

  • Print
Details
Published: 05 January 2023

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt.  Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 05/01/2023 amefungua  kikao cha tathmini ya kazi za Dayosisi kwa mwaka 2022. Kikao kinafanyika katika hoteli ya Mbuyukenda Tanga.

Hits: 12124

Read more ...

Waziri wa Nishati atembelea Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki 

  • Print
Details
Published: 03 January 2023

Waziri wa Nishati, na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mhe.January Makamba amefika katika Ofisi za Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki leo tarehe 03/01/2023 na kutoa salamu zake za Mwaka Mpya, pongezi na shukrani kwa Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu kwa ushirikiano mkubwa anaouonyesha katika ngazi ya jamii na Serikali kwa ujumla.

 Mhe. January Makamba ameahidi kwamba wao kama viongozi wa Serikali wataendelea kutoa ushirikiano na kuunga mkono juhudi na mipango inayofanywa na KKKT-DKMs na Kanisa kwa ujumla ikiwemo kuona taasisi mpya ya KOTETI inainuka na kutimiza malengo makubwa mapya iliyopewa ya kuongeza ujuzi kwa watanzania kwa kozi ya ufamasia (Pharmacy)  na kozi mbalimbali zitakazo endelea kutolewa katika Chuo hicho cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kinacho milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Kwa upande wake Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mambo mengi ya maendeleo anayoyafanya sana sana mradi wa kufua Umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) ambao utasaidia katika upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuondoa tatizo la uhaba wa umeme nchini pamoja na kupunguza gharama za umeme kwa Watanzania.

Askofu Dkt. Mbilu ameipongeza serikali kwa juhudi walizozionyesha kupitia Waziri wa nishati Mhe. January Makamba/ Mbuge wa Bumbuli kwa ushirikiano waliouonyesha na kuwashika mkono katika mchakato wa kuanzisha Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI.) ambacho kwa sasa tayari kinatoa Kozi ya Ufamasia (Pharmacy) inayohusika na kuandaa, kuchanganya na kutoa dawa za kimatibabu kwenye mahospitali, maduka ya madawa, na viwandani.

Hits: 11844

Salamu za mwaka mpya 2023, za Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.

  • Print
Details
Published: 01 January 2023

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ametoa salamu za mwaka mpya wa 2023 kutoka kitabu cha Ayubu 22:21. “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. 

Askofu Dkt. Mbilu akihubiri katika Ibada ya Jumapili na mwaka mpya 2023 leo tarehe 01/01/2023 katika Jimbo la Kusini Usharika wa Vuga ametoa wito kwa washarika na wakristo kwa ujumla kufungua mawazo nakumjua Mungu zaidi katika mwaka huu wa 2023 ili mema yaambatane nao. “Mungu tunaye paswa kumjua zaidi na zaidi uso wake hautatuacha”.

MKUU WA JIMBO LA KUSINI: MCH. ISSAI MWETA

Kwa upande wake, Mkuu wa Jimbo la Kusini Mch. Issai Mweta pamoja na kuwasihi wana KKKT-DKMs kuendelea kuiombea Dayosisi amewakumbusha wakristo wote kuombea amani ya nchi pamoja na kudumisha umoja.

Hits: 11764

Salamu za Sikukuu ya Krismasi, 2022 KKKT-DKMs

  • Print
Details
Published: 25 December 2022

“Isaya 9:2 “Watu wale waliokwenda katika giza wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza.”

Hits: 12289

Read more ...

  1. Askofu Dkt. Mbilu awasihi vijana kugeuza mitandao ya kijamii kuwa fursa
  2. Semina elekezi kwa Sharikani za KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa mwaka 2023.
  3. Wakristo wa KKKT kutoka Ngorongoro wapokelewa rasmi KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
  4. Askofu Dkt. Msafiri Mbilu atoa wito kwa Kanisa kuwatambua viziwi

Page 63 of 137

  • 58
  • 59
  • ...
  • 61
  • 62
  • 63
  • 64
  • ...
  • 66
  • 67

Back to Top

© 2026 ELCT North Eastern Diocese