ELCT North Eastern Diocese
Mch. Emmanuel Mtoi atambulishwa Usharika wa Kana sasa kuliongoza Jimbo la Pwani.
- Details

KUTOKA USHARIKA WA KANA TANGA: Leo tarehe 15/01/2023, Msaidizi wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju ameongoza Ibada ya Jumapili katika Jimbo la Pwani Usharika wa Kana.
- Hits: 11417
Askofu Dkt. Mbilu afungua Kanisa na kuweka jiwe la msingi la Madarasa ya Watoto wa Shule ya Jumapili katika Usharika wa Magamba.
- Details

Leo tarehe 15/01/2023 imekuwa siku ya furaha na baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Magamba ambapo, Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akiwa katika Jimbo la Kusini,ameongoza Ibada ya Jumapili iliyotanguliwa na ufunguzi wa Kanisa katika Usharika wa Magamba Mtaa wa Mabughai pamoja na uwekwaji wa jiwe la msingi katika madarasa ya Watoto wa Shule ya Jumapili (Sunday School) katika senta ya Usharika huo wa Magamba.
- Hits: 11510
Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu aongoza Ibada ya mazishi ya Mch. Sabina Lumwe.
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewataka waumini kuishi maisha yanayofaa na kumpendeza Mungu katika ulimwengu huu na kuacha mambo yasiyofaa ili kuwa na mwisho mwema. Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo kwenye Ibada ya mazishi ya marehemu Mch. Sabina Lumwe na kusema kuwa marehemu Mch. Sabina lumwe alisimama vyema katika utumishi wake.
- Hits: 13400
Pumzika kwa amani Mch. Sabina Lumwe
- Details
Kristo anasema: "KILA ANIAMINIYE AJAPOKUFA ATAKUWA ANAISHI."
Askofu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazani Mashariki Mch. Dkt Msafiri Joseph Mbilu ,anasikitika kutangaza kifo cha Mch. Sabina Lumwe kilichotokea leo tarehe 08/01/2023 nyumbani kwake Lushoto. Ibada ya mazishi itafanyika siku ya jumanne ya tarehe 10/01/2023 Kanisa Kuu (cathedral) Lushoto na itaanza saa 4:00 asubuhi.
- Hits: 11765
Page 62 of 137

