ELCT North Eastern Diocese
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Muheza , Youths Confirmation at Muheza Lutheran Parish
- Details
KATIKA PICHA: Ibada ya Jumapili ya tarehe 15/10/2023 kutoka Jimbo la Tambarare Usharika wa Muheza. Ibada hii iliongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ilikuwa na tendo la kuwabariki vijana wa Kipaimara. Pamoja na hayo Vijana hao waliobarikiwa wamemshukuru Mhashamu Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu kwa kufundishwa neno la Mungu kwa kipindi cha miaka miwili huku wakitoa pongezi kwa kazi mbalimbali za maendeleo zinazofanyika ndani ya Dayosisi chini ya uongozi wa Baba Askofu Dkt. Mbilu.
- Hits: 9896
Askofu Dkt. Mbilu afanya mazungumzo na kuagana na wanafunzi wa Theologia
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewapongeza nakuwatakia baraka za Mungu katika masomo yao wanafunzi wanaoenda masomoni kwa mhula mpya wa masomo na wale ambao wanaendelea na masomo katika Chuo cha Biblia na Theolojia Mwika pamoja na Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira.
- Hits: 9314
Askofu Dkt. Mbilu azindua Jimbo la 5 ndani ya KKKT-DKMs, amuingiza kazini Mkuu wa Jimbo pamoja na Katibu Mkuu wa Dayosisi.
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameongoza Ibada iliyokuwa na tendo la kuzindua Jimbo la tano ndani ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Ibada hiyo pia iliambatana na kuingizwa kazini kwa Mkuu wa Jimbo hilo Mch. Ishmael Reuben Ngoda pamoja na Katibu Mkuu wa Dayosisi Mwl. Julius Samwel Madiga .
- Hits: 9789
Page 45 of 137


