ELCT North Eastern Diocese
Askofu wa KKKT-DKMs Dkt. Msafiri Mbilu apokea wadiakonia 30 kutoka Ujerumani
- Details

MATUKIO KATIKA PICHA TAREHE 02/11/2023:- Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu pamoja na kikundi cha Wadiakonia 30 kutoka Ujerumani ambao wameitembela Dayosisi yetu na wamepata nafasi ya kutembelea shule ya Msingi ya Irente Rainbow School inayomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.Baba Askofu amewashukuru wadiakonia hawa wenyeurafiki na shule hii kwa namna wanavyojitoa kwa hali na mali katika kuchangia maendeleo ya shule hiyo.Katika kuchangia maendeleo na kazi mbalimbali katika shule hiyo wadiakonia hawa wametoa kiasi cha Tsh: 7,891,200.
- Hits: 9580
Pumzika kwa amani Mchungaji Mpewa Lazaro Ruwa
- Details
Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu tarehe 01/11/2023 ameongoza Ibada ya mazishi ya marehemu Mch. Msataafu Mzee Mpewa Lazaro Ruwa iliyofanyika katika Jimbo la Pwani Usharika wa Makorora Tanga.
Marehemu Mzee Ruwa aliitwa mbinguni tarehe 28/10/2023 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo na mwili wake umepumzishwa tarehe 01/11/2023 katika makaburi yaliyopo katika eneo la Gofu Tanga.
- Hits: 9540
Ziara ya Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, nchini Tanzania.
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,ni mmoja wa wageni walioalikwa kwenye hafla ya Chakula cha Jioni iliyoandaliwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania . Hafla hii ilifanyikia tarehe 31/10/2023 katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Jijini Dar es Salaam ikiwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo wenye ushirikiano na Ujerumani.Hapa Baba Askofu Dkt. Mbilu alialikwa kwa mwaliko maalumu kutokana na uhusiano mkubwa uliopo na wa muda mrefu kati ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Ujerumani.

- Hits: 9352
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Tamota, Youths Confirmation at Tamota Lutheran Parish
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki amewashukuru washarika wa Usharika wa Tamota na wanadayosisi kwa ujumla kwa namna wanavyoendelea kushikamana na kujitoa katika kumtumikia Mungu.
- Hits: 8797
Page 43 of 137

