ELCT North Eastern Diocese
Toggle Navigation
  • Home
  • Our Diocese
  • Wopa
  • Gallery
  • Institutions
    • Irente Children's Home
    • Irente School for the Blind
    • Rainbow School
    • Lwandai Secondary School
    • Lutindi Mental Hospital
    • Bangala Lutheran Junior Seminary
    • Bumbuli Hospital
    • SEKOMU university
    • Namna ya kuchangia kazi za maendeleo na Vituo vya kutoa huduma kwa watu wenye mahitaji maalumu (KKKT-DKMs)
  • Calendar
  • Projects
    • Irente Biodiversity Reserve
    • UTC - Usambara Technological Center
    • Restaurants and Hostels
      • Tumaini Mbuyukenda Hostel and Restaurant
      • Martin Luther Garden and Restaurant
      • Tumaini Songe Restaurant and Hostel
      • Hohen Restaurant and Hostel
      • Tumaini Lushoto Restaurant and Hostel
  • Superintendent
    • Coast Superintendent
    • Northern Superintendent
    • Southern Superintendent
    • Plains Superintendent
  • New-clips
  • Contact us
  • You are here:  
  • Home

Bishop Rev.Dr. Msafiri J. Mbilu

Change Language

English German Spanish Swahili Swedish

News & Updates

  • TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI YA KAZI Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya...
  • Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji  NSSF

    Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF

    Leo tarehe 01/04/2026, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amepokea ugeni kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifa...
  • TAARIFA

    TAARIFA

    Uongozi wa KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ukiwakilishwa na Katibu Mkuu Mwl. Julius Madiga, u...
  • ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Dkt. Msafiri Jos...
  • Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Dayosisi yetu imepata heshima kubwa ya kushiriki katika Mkutano wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na U...

.



 

 

Staff Email

ELCT North Eastern Diocese

Kuelekea Harambee kubwa ya kuchangia kazi za maendeleo na vituo vya Diakonia KKKT-DKMs

  • Print
Details
Published: 04 August 2023

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ametoa wito kwa wafanyabiashara, wadau mbalimbali wa elimu na maendeleo pamoja na Watanzania kwa ujumla kuungana na KKKT-DKMs kwenye harambee kubwa yenye lengo la kuchangia kazi za maendeleo na Vituo vya Diakonia vya  KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki itakayofanyika tarehe 18/08/2023 Jijini Dar Es Salaam.

Hits: 10323

Read more ...

Familia ya Askofu Dkt. Mbilu watoa Sadaka ya Shukrani  yaelekezwa kulipa Deni la Dayosisi.

  • Print
Details
Published: 16 July 2023

Jumapili ya leo tarehe 16/07/2023 imekuwa siku ya furaha na baraka tele kwa familia ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ambaye akiambatana na familia yake, wamemtolea Mungu sadaka ya shukrani kwa namna Mungu alivyomtetea Binti yao Sarah hasa wakati wa Ugonjwa wa CORONA.

Katika Ibada iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto,ikiongozwa na Baba Askofu Jacob Ole Moreto Paulo Mameo wa KKKT-Dayosisi ya Morogoro. Askofu Dkt. Mbilu amesema kuwa yeye na familia yake wanawiwa kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyomlinda Binti yao Sarah katika kipindi chake cha Masomo cha miaka 6 nchini China. "Lililokubwa kwetu kama Familia ni kuona jinsi Mungu alivyomtetea Binti yetu hasa wakati wa Ugonjwa mbaya wa CORONA ambao ulianzia pale Wuhan kwenye Chuo ambacho alikuwa anasoma binti yetu.

Wakati wa CORONA tulijaribu kumuondoa Sarah arudi nyumbani lakini tulishindwa kabisa. Pale tuliposhindwa tulinyoosha mikono na kumuachia Mungu, leo mioyo yetu imejaa furaha kubwa tunapoona Sarah amemaliza masomo yake ya Shahada ya kwanza ya Utabibu (Bachelor of Medicine) na kurejea nyumbani salama. Katika furaha hii tumeona tumtolee Mungu Shukrani ya pekee" Amesema Askofu Dkt. Mbilu.

Sadaka iliyopatikana katika Ibada hiyo ya Shukrani ilikuwa fedha taslim Milioni nne na elfu sita (Tsh. 4,006,000), ahadi Milioni tatu na laki nane (Tsh. 3,800,000/=) na kufanya jumla kuu kuwa shilingi Milioni Saba laki nane na elfu sita (7,806,000). Kiaisi hiki kilicho patikana kimeelekezwa  kulipia deni kubwa la Dayosisi.Askofu Dkt. Msafiri Mbilu amewashukuru ndugu jamaa na marafiki waliofanikisha kupatika kwa kiasi hicho kitakacho saidia katika ulipaji wa Deni la Dayosisi.

Hits: 11835

Katibu Mkuu wa KKKT Mhandisi Robert Kitundu awataka Wakristo kuliombea Kanisa

  • Print
Details
Published: 09 July 2023

Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Mhandisi Robert Kitundu amewataka Wakristo wa KKKT kuendelea kuliombea Kanisa na kulisogeza mikononi mwa Mungu ili liendelee kudumu katika Umoja na upendo wa kweli.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo leo tarehe 09/07/2023 kwenye Ibada ya Jumapili iliyofanyika  KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Magharibi Usharika wa Kimara ambapo pamoja na kuliombea Kanisa  amewasihi Wakristo kutunza Ulutheri katika kumtukuza Mungu.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt.Msafiri Joseph Mbilu ambaye yupo katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi anayoifanya KKKT-DMP ni mmoja wa walio shiriki katika Ibada hii.

Mchana wa leo Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu atakuwa na mkutano na   Wakristo wote wanaotokea KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto, Tanga pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo waishio Dar es Salaam kuanzia saa 9:00 Alasiri. Mkutano huu utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano KKKT - Mbezi Beach.

 

Hits: 11414

Dean  Michael Kanju akabidhi pikipiki kwa Chuo cha Biblia Vuga.

  • Print
Details
Published: 04 July 2023

Msaidizi wa Askofu wa KKKT-DKMs Mch Michael Kanju (Kushoto) akimakabidhi Mkuu wa Chuo cha Biblia Vuga Mch. Benson Kimweri Kivuli cha kadi ya Pikipiki

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju amekabidhi pikipiki 1 kwa Mkuu wa Chuo cha Biblia Vuga Mch. Benson Solomon Kimweri, ikiwa ni hatua za awali za kutatua changamoto ya usafiri  Chuo hapo huku akiagiza pikipiki hiyo kwenda kutumika kwa malengo mahsusi yaliyokusudiwa,

Mzaidizi huyo wa  Askofu Mch. Michael Kanju amekabidhi pikipiki hiyo kwa niaba ya Baba Askofu Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 04/07/2023 katika Makao Makuu ya KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto Tanga.

Hii ni kufuatia ahadi ya Askofu Dkt. Msafiri Mbilu  aliyoitoa mnamo tarehe 28/06/2023  akiwa katika ziara yake ya kikazi kutoa pikipiki kwa ajili ya Chuo hicho cha Biblia Vuga ambapo pia aliueleza uongozi wa Chuo hicho kuwa mipango ya  upatikanaji wa gari kwaajili ya  Chuo hicho bado inaendelea.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Mch. Benson   Kimweri  ameushukuru uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kuwapatia pikipiki hiyo itakayokuwa msaada katika mambo ya usafiri.

Hits: 11053
  1. Ungana nasi kuchangia Deni la Dayosisi
  2. UNGANANASI KUCHANGIA DENI LA DAYOSISI ILI KUNUSURU MALI ZA DAYOSISI ZISIPIGWE MNADA.
  3. Askofu Dkt. Mbilu aanza ziara na ujumbe kutoka Bethel-Ujerumani.
  4. Awamu ya tatu uchangiaji deni la Dayosisi kunusuru mali zisipigwe mnada

Page 49 of 137

  • 44
  • ...
  • 46
  • 47
  • 48
  • 49
  • ...
  • 51
  • 52
  • 53

Back to Top

© 2026 ELCT North Eastern Diocese