ELCT North Eastern Diocese
TANGAZO LA KAZI MTEKNOLOJIA DARAJA II-DAWA
- Details
KANISA LA KINJIILI LA KILUTHER TANZANIA
DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI
S.L.P 10,
LUSHOTO.
NAFASI YA KAZI
Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni miongoni mwa Dayosisi 27 ndani ya KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-DKMs ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi ifuatayo:
MTEKNOLOJIA DARAJA LA II-DAWA (NAFASI 1)
MAJUKUMU YA MUOMBAJI
- Kuanisha, kuandaa na kuagiza mahitaji ya dawa na vifaa tiba katika eneo la kazi.
- Kugawa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa na watumishi.
- Kuchanganya dawa.
- Kuhifadhi dawa na vifaa tiba.
- Kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya dawa.
- Kukagua dawa, vifaa tiba kemikali, vitendanishi na vipodozi katika eneo lake la kazi.
- Kutoa taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa.
- Kuratibu kazi za kamati ya dawa na vifaa tiba.
- Kuandaa taarifa ya matumizi ya dawa na vifaa tiba.
- Kufanya uchunguzi wa ubora wa dawa, vifaa tiba kemikali, vitendanishi na vipodozi.
- Kufanya kaguzi mbalimbali katika sehemu zinazohifadhi dawa.
- Kusimamia utendaji kazi watumishi walio chini yake.
- Kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba.
SIFA ZA MWOMBAJI
- Elimu ya kuanzia Diploma ya ufamasia kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
- Lazima
- Ajue kutumia software za computer Zaidi kipengele cha Microsoft office.
- Ajue kutumia software zinatumika katika usimamiaji wa dawa.
- Mwenye moyo wa kufanya kazi kwenye mazingira yoyote.
- Umri kuanzia miaka 25 na isiyozidi 40
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.
- Barua ya maombi iambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu, wasifu wa mwombaji (Cv), cheti cha kuzaliwa, na nakala za vyeti vyote vya ujuzi mbalimbali (kama unavyo).
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 24/11/2023
- Waombaji watakaokidhi vigezo ndio watakaoitwa kwenye usaili (Interview)
Tarehe ya usaili watajulishwa kwa njia ya simu.
Maombi yote yatumwe kwa Katibu Mkuu-KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki S.L.P 10 LUSHOTO Au: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
- Hits: 10217
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Ubiri , Youths Confirmation at Ubiri Lutheran Parish
- Details










- Hits: 9273
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Ambangulu , Youths Confirmation at Ambangulu Lutheran Parish
- Details








- Hits: 8922
Kuelekea kilele cha kuchangia Deni la Dayosisi kwa awamu ya Tsh. 30,000 kwa kila Msharika wa KKKT-DKMs
- Details

Kuelekea kilele cha uchangiaji wa Tsh 30,000 kwa kila msharika wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki-(KKKT-DKMs) kwa ajili ya kupunguza deni linaloikabili Dayosisi kitakacho fanyika katika Jimbo la Tambarare Usharika wa Korogwe tarehe 17/12/2023. Askofu Dkt Msafiri Mbilu amewashukuru wale wote ambao wameingia kazini kuchangia deni hilo.
Askofu Dkt. Mbilu ameongeza kuwa siku hiyo itakuwa ni kilele cha kukusanya kiasi hicho na kupata taarifa za uchangiaji kwa kila Usharika “Awali ya yote napenda kuwashukuru ninyi wote kwa jinsi mlivyopokea wito huu wa kila mmoja kuchangia Tsh. 30,000/=. Fedha hizi zimesaidia sana kupunguza deni la Dayosisi. Ninapenda kuwajulisha kuwa tutakuwa na siku rasmi ya kilele cha mchango huu wa Tsh. 30,000 tarehe 17/12/2023 kwenye Jimbo la Tambarare Usharika wa Korogwe, wapo watu wengi waliomaliza na kuendelea kuongeza zaidi na zaidi patano la kuchangia kiasi cha Tsh.30,000, lakini pia wapo ambao wameanza lakini hawajakamilisha nawasihi kukamilisha patano letu".Alisema Askofu Dkt. Mbilu.
Baba Askofu amesisitiza kwa wale wote ambao bado hawajakamilisha mchango wa Tsh. 30,000/= wanaombwa kukamilisha mchango wao kupitia Sharika zao ili siku ya kilele taarifa ya kila Usharika iwasilishwe bila deni, ili kutoa mwanga wa jinsi ya kujipanga na awamu nyingine za uchangiaji.
Kutokana na ukubwa wa deni la Dayosisi harambee hizi zitakuwa endelevu,Baba Askofu anazidi kuwatakia baraka za Mungu ninyi nyote kwa kujitoa kwenu ili kazi ya Mungu iendelee kusonga mbele kwani kwa mshikamano uliopo ipo siku deni hili litakwisha na kurudisha heshima ya Dayosisi yetu.
- Hits: 10160
Page 42 of 137

