ELCT North Eastern Diocese
Toggle Navigation
  • Home
  • Our Diocese
  • Wopa
  • Gallery
  • Institutions
    • Irente Children's Home
    • Irente School for the Blind
    • Rainbow School
    • Lwandai Secondary School
    • Lutindi Mental Hospital
    • Bangala Lutheran Junior Seminary
    • Bumbuli Hospital
    • SEKOMU university
    • Namna ya kuchangia kazi za maendeleo na Vituo vya kutoa huduma kwa watu wenye mahitaji maalumu (KKKT-DKMs)
  • Calendar
  • Projects
    • Irente Biodiversity Reserve
    • UTC - Usambara Technological Center
    • Restaurants and Hostels
      • Tumaini Mbuyukenda Hostel and Restaurant
      • Martin Luther Garden and Restaurant
      • Tumaini Songe Restaurant and Hostel
      • Hohen Restaurant and Hostel
      • Tumaini Lushoto Restaurant and Hostel
  • Superintendent
    • Coast Superintendent
    • Northern Superintendent
    • Southern Superintendent
    • Plains Superintendent
  • New-clips
  • Contact us
  • You are here:  
  • Home

Bishop Rev.Dr. Msafiri J. Mbilu

Change Language

English German Spanish Swahili Swedish

News & Updates

  • TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI YA KAZI Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya...
  • Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji  NSSF

    Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF

    Leo tarehe 01/04/2026, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amepokea ugeni kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifa...
  • TAARIFA

    TAARIFA

    Uongozi wa KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ukiwakilishwa na Katibu Mkuu Mwl. Julius Madiga, u...
  • ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Dkt. Msafiri Jos...
  • Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Dayosisi yetu imepata heshima kubwa ya kushiriki katika Mkutano wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na U...

.



 

 

Staff Email

ELCT North Eastern Diocese

Mchango wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kuelekea uzinduzi wa Dayosisi ya Magharibi

  • Print
Details
Published: 08 October 2022

Mchango wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kuelekea uzinduzi wa Dayosisi ya Magharibi - KIGOMA HAPO KESHO TAREHE 09/10/2022.

Wakristo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, waliokuwa wanafanya kazi Mkoani Kigoma, walijikusanya chini ya uongozi wa ndugu. Edward Kiswaga aliyekuwa mtumishi wa Uhamiaji. Waliandika barua yao Makao Makuu ya KKKT yaliyopo Mkoani Arusha kuomba wapatiwe Mchungaji atakaye wahudumia kwa taratibu za Kilutheri.

Wakati huo walikuwa wakijiongoza wenyewe wakisali katika chumba cha darasa katika shule ya msingi Muungano iliyoko Mwanga Kigoma. Kabla ya hapo walikuwa wakipewa huduma za kiroho na Mchungaji wa Kanisa la Moravian Kigoma.

Mkuu wa KKKT Hayati Askofu Dkt. Sebastian Kolowa na Katibu Mkuu wa KKKT ndugu. Joel Ngeiyamu wakati huo walipokea ombi la washarika wa Kilutheri Kigoma na kulipeleka kwa Halmashauri Kuu ya KKKT. Uamuzi wa Halmashauri Kuu ya KKKT ulikuwa kukabidhi Misioni ya Kigoma itunzwe na Dayosisi tatu zifuatazo kwa kupokezana kila baada ya miezi mitatu.

  • KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
  • KKKT-Dayosisi ya pare
  • KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Magharibi.

KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ilikuwa ya kwanza kuitikia haraka wito wa KKKT na kumtuma Mchungaji kigoma. Tarehe 4/4/1983 Mchungaji Msaidizi Zawadiel Joseph Mkilindi alibarikiwa kuwa Mchungaji katika Kanisa dogo la Usharika wa Lushoto na kutumwa Mkoani Kigoma.Mchungaji Zawadiel Joseph Mkilindi alikabidhiwa Usharika wa Kigoma na Katibu wa Misioni na Uinjilisti wa KKKT-DKMs Mch. Timilai Ismael Guga, katika Ibada iliyofanyika katika darasa la shule ya msingi muungano katika manispaa ya Kigoma Ujiji. Wakati huo Usharika ulikuwa na mitaa mitatu ambayo ni:- Kigoma mjini ,Kagunga Kaseke. Aidha palikuwa na kikundi cha kwaya ya vijana Kigoma Mjini.

WITO WA MAFUNDISHO YA UWAKILI NA KUJITEGEMEA.

Mchungaji Mkilindi aliwatia moyo Washarika wa Kigoma kwa kuweka mambo matatu mbele yao ambayo ni ya mkazo wa mafundishi ya uwakili na kujitegemea. Kwa kuinua moyo wa umoja, kujitoa na kujitolea kujenga ufalme wa Mungu kwa kutoa mali na vipawa vyao kwa hali ya juu; uinjilisti uliwezesha falsafa iliyosaidia kuendeleza kazi ya Bwana na kusaidia kusimama katika mambo matatu: - Kujitegemea- Self Reliance, Kujiongoza – Self Governing pamoja na Kujieneza - Self Propagation.

falsafa hii ilisaidia Washarika kujua kuwa kazi ya mungu iko mikononi mwao. hivyo watumie mali, hazina na vipaji vyao kujenga na kueneza ufalme wa mungu Mt. 28: 19-20, Mk 16:15.

Hata hivyo Mch Zawadiel Mkilindi kazi yake ya kwanza ilikuwa kuwatembelea wakristo kwa miguu majumbani na maofisini ili kufahamiana na kuwaimarisha kiroho, alitembea katika maeneo ya biashara ili wafanyabiashara nao wafike Kanisani. Ziara hizi zilijenga umoja na mshikamano katika Yesu Kristo na kupanua wigo wa mahudhurio Ibadani.

Huyu ndiye mmisionari wa kwanza wa KKKT-KIGOMA Mch Zawadiel Joseph Mkilindi.

Hits: 13282

Wito watolewa kujiunga na Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI)

  • Print
Details
Published: 25 September 2022

MSAIDIZI WA ASKOFU KKKT-DKMs, MCH MICHAEL MLONDAKWELI KANJU

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Michael Mlondakweli Kanju ametoa wito kwa wazazi na walezi kutuma watoto wao kujiunga na Chuo cha Kolowa Technical Training Institute kinachotoa Kozi ya Ufamasia (Pharmacy).

amesema kuwa ni vema kutumia muda wa udahili ulioongezwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kutuma maombi yao ilikujiunga na Chuo hicho.

Hits: 14505

Read more ...

Ibada ya Kipaimara Usharika wa Hengiti ,, Youths Confirmation at Hengiti Lutheran Parish

  • Print
Details
Published: 24 September 2022

Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Godfrey Tahona Walalaze leo Jumamosi ya tarehe 24/09/2022 ameongoza Ibada ya Kipaimara iliyofanyika katika Usharika wa Hengiti Mtaa wa Fuizai

ambapo jumla ya vijana wapatao 108 wamepata kipaimara huku wakikiri kufundishwa na kuifahamu misingi ya imani yao na kuahidi kuto yumbishwa na mafundisho  ya uongo .

Hits: 12319

Read more ...

Mwendelezo wa Ziara ya kikazi ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu nchini Ujerumani

  • Print
Details
Published: 21 September 2022

\

Sehemu ya Wajumbe wengine wa Kamati ya Uhusiano

PICHA YA PAMOJA mara baada ya mazungumzo ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu na Mkuu wa Jimbo la Vlotho Mch. Dorothea Goudefroy (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wajumbe  wa kamati ya Undugu toka Vlotho.

Hits: 12372

Read more ...

  1. Ziara ya kikazi ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, Nchini Ujerumani
  2. Siku ya baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Malibwi Jimbo la Kaskazini.
  3. Mkutano wa Wachungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilitutheri Tanzania wafunguliwa Dodoma
  4. Tangazo la nafasi ya kazi Meneja wa Hoteli (Hotel Manager)

Page 70 of 137

  • 65
  • 66
  • 67
  • 68
  • 69
  • 70
  • 71
  • 72
  • 73
  • 74

Back to Top

© 2026 ELCT North Eastern Diocese