ELCT North Eastern Diocese
Washa ya viongozi wa Makanisa wanachama wa UEM Afrika nzima
- Details
MATUKIO KATIKA PICHA:-Washa ya viongozi wa Makanisa wanachama wa UEM kwa ukanda wa Afrika nzima. Washa hii inayofanyika Katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam, mkazo wake nikuona jinsi ya kuweka mipango thabiti mara baada ya kustaafu kwa watumishi wa Kanisa. Katika semina hiyo masomo mengi yamefundishwa yakionyesha mifano mbalimbali ya jinsi watumishi wa Kanisa wanavyotunzwa wanapostaafu huko Ulaya (Ujerumani), Asia na Afrika. Pamoja na mambo mbalimbali yaliyo fundishwa na kujadiliwa katika semina hiyo, pia washiriki wamejengewa uwezo na ufahamu wa pamoja kwa kuona ni kwa jinsi gani Makanisa yanaweza kushirikiana kujengeana uwezo mapema wa namna ya kuwatunza Wastaafu.

- Hits: 10332
KATIKA PICHA IBADA YA NDOA KATI YA MHANDISI ANJAWE TURUCK NYAGAWA NA DKT. SARAH MSAFIRI MBILU
- Details
MATUKIO KATIKA PICHA,IBADA YA NDOA KATI YA MHANDISI ANJAWE TURUCK NYAGAWA NA DKT. SARA MSAFIRI MBILU, IBADA IMEFANYIKA KATIKA USHARIKA WA MBEZI BEACH KKKT-DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI NA ILIONGOZWA NA MKUU WA KKKT MTEULE BABA ASKOFU DKT. ALEX MALASUSA . TAREHE 13,01,2024. DKT. SARA NI MTOTO WA KWANZA WA ASKOFU WA KKKT-DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI MCH DKT. MSAFIRI JOSEPH MBILU.

- Hits: 9903
Heri ya Mwaka Mpya 2024 , Tuanze yote katika Jina la Yesu Kristo
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewataka Wazazi na Walezi wanapo upokea mwaka Mpya wa 2024 kuendelea kuwalea Watoto wao katika maadili mema kwani malezi bora ndiyo msingi wa kumsaidia Mtoto kutimiza malengo yake ya mbeleni.
- Hits: 11584
Page 37 of 137


