ELCT North Eastern Diocese
Toggle Navigation
  • Home
  • Our Diocese
  • Wopa
  • Gallery
  • Institutions
    • Irente Children's Home
    • Irente School for the Blind
    • Rainbow School
    • Lwandai Secondary School
    • Lutindi Mental Hospital
    • Bangala Lutheran Junior Seminary
    • Bumbuli Hospital
    • SEKOMU university
    • Namna ya kuchangia kazi za maendeleo na Vituo vya kutoa huduma kwa watu wenye mahitaji maalumu (KKKT-DKMs)
  • Calendar
  • Projects
    • Irente Biodiversity Reserve
    • UTC - Usambara Technological Center
    • Restaurants and Hostels
      • Tumaini Mbuyukenda Hostel and Restaurant
      • Martin Luther Garden and Restaurant
      • Tumaini Songe Restaurant and Hostel
      • Hohen Restaurant and Hostel
      • Tumaini Lushoto Restaurant and Hostel
  • Superintendent
    • Coast Superintendent
    • Northern Superintendent
    • Southern Superintendent
    • Plains Superintendent
  • New-clips
  • Contact us
  • You are here:  
  • Home

Bishop Rev.Dr. Msafiri J. Mbilu

Change Language

English German Spanish Swahili Swedish

News & Updates

  • TAARIFA

    TAARIFA

    Uongozi wa KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ukiwakilishwa na Katibu Mkuu Mwl. Julius Madiga, u...
  • ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Dkt. Msafiri Jos...
  • Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Dayosisi yetu imepata heshima kubwa ya kushiriki katika Mkutano wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na U...
  • Contact Us

    Contact Us

    SOUTHERN SUPERINTENDENT BARUA PEPE JIMBO LA KUSINI southern.superintendent@elctned.org cathedral@elc...
  • Askofu Dkt. Mbilu afungua Kikao Kazi cha Tathmini ya Mwaka 2025

    Askofu Dkt. Mbilu afungua Kikao Kazi cha Tathmini ya Mwaka 2025

    Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Jos...

.



 

 

Staff Email

ELCT North Eastern Diocese

Askofu Dkt. Mbilu kila Makristo anaowajibu wa Kushuhudia Nuru na Upendo wa Kweli wa Yesu Kristo

  • Print
Details
Published: 31 July 2025

MAKAYO KOROGWE: Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) amewataka Wakristo kuacha kufuata mafundisho potofu na badala yake wachukue jukumu la kuyashuhudia Maandiko Matakatifu kwa wengine.

Akizungumza Alhamisi, Julai 31, 2025, wakati wa Ibada ya Kipaimara iliyofanyika katika Jimbo la Magharibi, Usharika Mteule wa Msomera, Mtaa wa Makayo, Askofu Dkt. Mbilu alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kushuhudia nuru ya kweli na upendo wa Yesu Kristo.

Askofu Dkt. Mbilu amewataka washarika wa Mtaa wa Makayo, ambao wengi wao ni jamii ya wafugaji wa Kimasai, kuacha kuwasikiliza watu wanaokwenda maeneo yao na kudai kuleta "nuru ya Wamasai," akisisitiza kuwa Yesu anatosha na yeye ndiye Nuru ya Ulimwengu. Aliwahimiza kuiga mfano wa Yesu Kristo, ambaye aliupenda ulimwengu wote na hakuja kwa ajili ya Wamasai pekee bali kwa ajili ya ulimwengu mzima.

Katika Ibada hiyo ilitanguliwa na ufunguzi wa Kanisa la Usharika Mteule wa Msomera, Mtaa wa Makayo. Jumla ya vijana 64 walibarikiwa na walichangia Tsh. 310,000 na mara baada ya  kuungwa mkono na wanaume na wanawake waliohudhuria Ibada hiyo, jumla ya shilingi 585,000 zilipatikana na zitaelekezwa katika ulipaji wa deni la Dayosisi.

 

Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii

INSTAGRAM - / elctned
FACEBOOK ACCOUNT North Eastern Diocese
FACEBOOK PAGE - ELCT-North Eastern Diocese
YOUTUBE - / KKKT DKMS Online TV
WEBSITE: www.elctned.org
KWA MAONI NA USHAURI:
Simu : +255 743 399 798
Hits: 6142

Tangazo la nafasi ya kazi Irente Farm

  • Print
Details
Published: 30 July 2025

KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA

DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI

S.L.P 10, (SIMU 027-266002 / Fax 027-2660092), LUSHOTO.

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

TANGAZO LA KAZI NAFASI YA BWANA SHAMBA KITUO CHA IRENTE FARM

Irente Farm ni kituo cha kilimo kinachomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT–DKMs), kilichopo Lushoto, Mkoani Tanga. Kituo hiki ni sehemu ya huduma za maendeleo ya jamii zinazotekelezwa na Dayosisi kupitia miradi ya kilimo endelevu. Katika kuimarisha ufanisi wake, kituo kinatangaza nafasi ya kazi kwa cheo cha Bwana Shamba. Tunakaribisha maombi kutoka kwa watu wenye sifa, uwezo, na maadili mema ya Kikristo kushiriki katika huduma hii muhimu.

Majukumu ya Msingi:

  • Kusimamia shughuli zote za kilimo katika shamba la Irente.
  • Kupanga, kuratibu na kufuatilia shughuli za uzalishaji wa mazao na ufugaji.
  • Kusimamia matumizi bora ya rasilimali za shamba (wafanyakazi, vifaa, mbegu, mbolea n.k).
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu mbinu bora za kilimo na ufugaji.
  • Kuandaa ripoti za maendeleo ya kilimo kwa uongozi wa Irente Farm.
  • Kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya kilimo.

Sifa za Mwombaji:

  • Awe na shahada (degree) katika Kilimo au fani zinazohusiana, kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
  • Awe na uzoefu wa angalau miaka miwili (2) katika kusimamia shughuli za kilimo na ufugaji.
  • Awe na uwezo wa kutumia kompyuta na kuandaa ripoti za kazi.
  • Awe tayari kuishi na kufanya kazi Irente – Lushoto.

 Namna ya Kutuma Maombi:

Maombi yote yaambatane na:

  • Barua ya maombi
  • Wasifu binafsi (CV)
  • Nakala ya vyeti vya kitaaluma
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa au NIDA

Maombi yote yatumwe   kwa:


Katibu Mkuu,
KKKT– Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,
S.L.P 10,
LUSHOTO – TANGA

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Mwisho wa Kutuma Maombi: Tarehe 15 Agosti 2025 (saa 9:59 alasiri)

Kumbuka:

Ni waombaji waliokidhi vigezo watakaoitwa kwenye usaili. Kanisa linahimiza usawa wa kijinsia – Wanawake pia wanahamasishwa kuomba nafasi hii.

 

 

Hits: 5500

Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Halmashauri Kuu ya KKKT-DKMs

  • Print
Details
Published: 28 July 2025

Hits: 5663

Read more ...

Ufunguzi wa Kanisa KKKT-Dayosisi ya Pare Usharika wa Same

  • Print
Details
Published: 27 July 2025

Hits: 5736
  1. Msaidizi wa Askofu Atoa Wito kwa Halmashauri Mpya ya Mipango na Fedha KKKT-DKMs
  2. Askofu Dkt. Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa juu wa UEM
  3. Mwendelezo wa Ziara ya kikazi ya Askofu Dkt. Msafiri Mbilu, nchini Ujerumani
  4. Ziara ya kikazi ya Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, nchini Ujerumani

Page 7 of 136

  • 2
  • 3
  • 4
  • ...
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • ...
  • 11

Back to Top

© 2026 ELCT North Eastern Diocese