×

Warning

Failed deleting thumb_115_722.jpg

Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania . Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yenye Makao Makuu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ni miongoni mwa Dayosisi 28 za KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri za kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu wote. Taasisi hii KUPITIA COMPASSION  inatangaza nafasi moja ya kazi ya Mtendakazi wa Huduma ya Kunusuru Maisha ya Mama na Mtoto.

SIFA ZA MTENDAKAZI WA HUDUMA YA KUNUSURU MAISHA YA MAMA NA MTOTO

NAFASI: Mtenda kazi katika Huduma ya Kunusuru Maisha ya mama na mtoto (HBI).

 MAHALI: Kituo cha huduma ya mtoto na kijana.

KUWAJIIBIKA: Atawajibika kwa Mratibu wa kituo cha huduma ya maendeleo ya mtoto na kijana.

Muhtasari wa majukumu ya kazi kwa mtendakazi

Mtendakazi wa huduma ya afua ya kunusuru maisha ya mama na mtoto kwa huduma za nyumbani (Survival & Sponsorship Home Based) atahusika moja kwa moja na akina mama na watoto watakaonufaika na huduma hii. Atatumia asilimia 80% ya muda wake wa kazi kwa kuwatembelea akina mama hao nyumbani kwao na kutoa mafunzo kwa kutumia mitaala mbalimbali ya  afua hii. Yeye ndiye atawajibika kutekeleza afua akishirikiana na watendakazi wengine katika kuhakikisha masuala yote katika program ya afua ya mama na mtoto yanatekelezwa. Ni jukumu la mtendakazi kufuatilia mwenendo wa namna  malengo ya afua ya mama na mtoto yatakavyosababisha tofauti kwa walengwa katika maisha ya kila siku Mtendakazi atafuatilia na kuhakikisha upimaji wa ukuaji wa mtoto unafanyika kila mwezi kwa utaratibu  uliowekwa na kuingiza taarifa kwenye mfumo wa mawasiliano wa Connect.  Awe ni mfano wa kuigwa katika ukristo wake, anayeheshimu watu na mwenye kutunza siri za watu.

 AWajibu na sifa za kipekee za mtendakazi

  Awe Mwanamke Mkristo, shahidi mwaninifu anayemshuhudia Yesu  na mpole akionyesha mwenendo kama Yesu alivyoonyesha katika kushughulikia  matatizo  ya watu ndani na nje ya kanisa.

  1. Afanye kazi kutokana na wito wa ndani, akitenda kama msemaji wa watoto na mama zao au walezi waishio katika umaskini na hawana uwezo wa kujisemea wenyewe (huduma zote kuhusiana na afya  ya mama na mtoto).
  2. Kuwatembelea akina mama mara mbili kwa mwezi kwenye kila kaya na mara moja kwa mwezi ni shuhuli za vikundi ili kufuatilia mambo atakayowafundisha kama yanatekelezwa.
  3. Kufundisha akina mama kuhusu namna bora yakulea watoto wao kama njia ya kuboresha maendeleo ya ukuaji wa watoto kwa akina mama walioandikiswa chini ya afua  ya kunusuru maisha ya mtoto katika kiwango cha familia.
  4. Atashiriki pamoja na watendakazi wengine katika kuandaa mpango kazi na bajeti ya Afua ya kunusuru maisha ya mtoto na wale wa ufadhili kwa huduma ya nyumbani wa mwaka, miezi mitatu, wiki na siku pamoja na kupanga bajeti ya shughuli zote kwa mwaka mzima akishirikiana na watendakazi wengine wa huduma ya mtoto chini ya uongozi mahiri wa Mratibu wa kituo. Atahakikisha kwamba ripoti ya majumuisho ya shughuli zote inaandaliwa kwa wakati uliopangwa na kuingiza kwenye mfumo wa Connect.
  5. Kuingiza taarifa sahihi kwenye Connect zinazohusu kitengo cha mama na mtoto, maendeleo ya makuzi, changamoto za kiafya na kufanya tathmini kwa watoto kwa wakati muafaka.
  6. Kutembelea nyumbani na katika shughuli za vikundi zinazo hamasisha  mchakato mzima wa kuyatambua mahitaji ya mama na mtoto na kutoa maono katika kuwezesha wamama kujikwamua kiuchumi.
  7. Atakuwa muhimili kwa kitengo cha afya ya watoto wachanga na wenye umri wa mwaka hadi miaka mitano kituoni kwa kushauri na kutoa tathmini ya maendeleo ya afya ya watoto wote  kwa kila robo ya mwaka.

 B. Uzoefu, uwezo na  ujuzi wa kazi

  1. Awe Mkristo ambaye ni mfano katika kunena, kutenda na mwenendo anayeonesha wito wake katika huduma ya Kikristo.
  2. Awe mwenye Stashahada au Shahada katika mojawapo ya fani zifuatazo; Uuguzi (Nursing), Utabibu (Clinical Officer), Chakula na Lishe (Food and Nutrition), Afya ya jamii (Public health) na/au Ustawi wa jamii (Community Development).
  3. Awe na umri kati ya miaka 25 hadi 45.
  4. Mwenye uzoefu katika mojawapo ya masuala yafuatayo:
  • Huduma za afya ya mama na mtoto kama kupima ukuaji wa mtoto,
  • Uelewa mpana kuhusu elimu ya unyonyeshaji na chanjo,
  • Elimu kuhusu lishe
  • Elimu kuhusu afya ya uzazi
  • Elimu kuhusu VVU na magonjwa mengine ya kuambukiza..
  1. Awe mbunifu na kutafuta kujifunza na kushirikiana na wadau wengine wa afya, malezi na wengine wanaohusika.
  2. Awe na utayari wa kujifunza.
  3. Awe tayari kutoa huduma wakati wowote inapotokea dharura.
  4. Wanawake wanahamasishwa kuomba nafasi hii.

 C. Matarajio kwa mtendakazi wa kituo kwa program za nyumbani

  Yafuatayo ni matarajio na sifa zinazotarajiwa kwa mtendakazi wa kituo wakati wa    utekelezaji wa mtaala wa programu ya nyumbani.

            Mtendakazi awe na uwezo/utashi wa:

  • Kujifunza kufanya kazi na watu wazima wenye elimu ya chini kabisa au wasiofahamu kabisa kusoma, kuandika au kuhesabu.
  • Awe na uwezo wa kujifunza maandalio ya masomo kabla au wakati wa utekelezaji kukidhi mahitaji na kile wanachopenda walengwa.
  • Kujifunza kuendeleza kile wanachopenda watu wazima wakati wa somo la kikundi

Mtendakazi aweze:

  • Kuvumilia na kuweza kusimamia mjadala wa mada nyeti kama vile mahusiano ya mume na mke, uwezekano wa unyanyasaji na utelekezaji, ndoa, ujauzito na kujifungua.
  • Kuvumilia ulazima wa kutembelea nyumbani kwa walengwa.
  • Kumsaidia mlengwa kuelewa neno la Mungu kwa namna inayoleta maana kwake.

Mtendakazi awe tayari:

  • Kutafiti au kuboresha andalio la somo. Mfano mtendakazi anaweza kuongeza muktadha kwa eneo husika katika kufundisha somo la shughuli za ujasiriamali.
  • Kujenga Imani kwa walengwa na kuonesha mfano wa kuigwa kwa tabia ambazo walengwa wanapaswa kuwa nazo. Mfano mtendakazi lazima anawe mikono kabla ya kushika chakula chochote ili kuonesha mfano kwa walengwa.

 Mtendakazi ni muhimu afahamu:

  • Viashiria vya walengwa ili kujua sababu inayopelekea malengo ya andalio la somo. Kila andalio la somo linahusiana na angalau kiashiria kimoja kwa mlengwa.
  • Mchakato wa tathmini kwa mlengwa.
  • Viashiria vya kanisa, mfadhili na kuweza kufahamu wigo mpana wa utekelezaji.
  • Mitindo mitatu ya msingi ya ujifunzaji, kusikia, kuona, kugusa na kujumuisha mitindo hii wakati wa ufundishaji wa maandalio ya somo.
  • Kwamba sehemu muhimu kabisa ya utekelezaji wa andalio la somo ni kufikia malengo. Sehemu iliyobaki ya andalio la somo inaweza kubadilishwa inapohitajika.

Eneo la kazi:

Mtendakazi atafanya kazi katika kituo cha ufadhili wa mtoto kwenye kanisa atakaloajiriwa. Kazi yake pia itahusisha shughuli za nje ya kituo kwa kuwatembelea nyumbani wale walengwa wa huduma ya kunusuru maisha ya mama na mtoto kwa kusudi la kuendesha mafunzo nyumbani na kwenye vikundi na kuwasaidia.

1.3 NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.

Maombi yote yatumwe kwa  

Katibu Mkuu KKKT-DKMs
S.L.P 10,
LUSHOTO TANGA
Kupitia email ya
:  This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

  • Barua ya maombi iambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu, Wasifu wa mwombaji (Cv), Cheti cha kuzaliwa, na nakala za vyeti vyote vya ujuzi mbalimbali (kama unavyo).
  • Barua ya utambulisho kutoka kwa Mchungaji wa Kanisa unaloabudia kwa sasa (Lazima)
  • Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15/09/2025
  • Waombaji watakaokidhi vigezo ndio watakaoitwa kwenye Usaili (Interview)
  • Tarehe ya Usaili watajulishwa kwa njia ya simu.