Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania . Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yenye Makao Makuu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ni miongoni mwa Dayosisi 28 za KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri za kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu wote. Taasisi hii KUPITIA COMPASSION INATANGAZA NAFASI MOJA YA MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA (CHILD AND YOUTH DEVELOPMENT CENTER COORDINATOR (CYDC).
Utangulizi Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana ni mwajiriwa wa Kanisa na atatumika katika Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana (KKKT – MKATA – TZ1211) kilichopo Sindeni – Wilaya ya Handeni.
1.1 MAJUKUMU
- Kuandaa Mpango wa mwaka wa Mshirika-Mwenza wa Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana kwa kushirikiana na wadau wote na kuwasilisha kwa Kamati ya Huduma ya Mtoto kwa uthibitisho na kuidhinishwa na uongozi wa Kanisa.
- Kuwasilisha taarifa ya kimaandishi ya Utendaji na Maendeleo ya Kituo kwa amati, Uongozi wa Kanisa na Huduma ya Compassion International Tanzania kama itakavyo takiwa kwa pande zote husika.
- Kuhakikisha kuwa taarifa zote za fedha na Watoto zinatunzwa vizuri na kuhuishwa kila mara zinapohitajika.
- Kushiriki katika zoezi la Usaili wa kuwapata watendakazi wengine wote wa Kituo kwa kutoa maoni ya kitaalamu kuhusu nafasi hizo.
- Kuhakikisha mazingira ya walengwa kituoni ni salama kwao kujifunza na kushiriki katika programu zote za Kituo.
- Kuhamasisha upatikanaji wa Raslimali za ndani kwa ajili ya Miundombinu inayohitajika kwa walengwa kujifunza.
1.2 SIFA ZA MRATIBU WA KITUO CHA MAENDELEO YA MTOTO NA KIJANA ELIMU:
Shahada ya Kwanza (kutoka kwenye Chuo kinachotambulika/kukubalika na Serikali).
Elimu katika maeneo ya Uongozi/Utawala, Usimamizi wa biashara, Maendeleo ya jamii, Maendeleo ya watoto, Theolojia, Ualimu na Sosholojia
1.3 NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.
Maombi yote yatumwe kwa
Katibu Mkuu KKKT-DKMs
S.L.P 10,
LUSHOTO TANGA
Kupitia email ya : This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
- Barua ya maombi iambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu, Wasifu wa mwombaji (Cv), Cheti cha kuzaliwa, na nakala za vyeti vyote vya ujuzi mbalimbali (kama unavyo).
- Barua ya utambulisho kutoka kwa Mchungaji wa Kanisa unaloabudia kwa sasa (Lazima)
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15/09/2025
- Waombaji watakaokidhi vigezo ndio watakaoitwa kwenye Usaili (Interview)
- Tarehe ya Usaili watajulishwa kwa njia ya simu.