
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ameongoza Ibada ya kuweka wakfu chombo cha usafiri (pikipiki) na kumkabidhi kadi ya pikipiki pamoja na ufunguo Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uchumi, Mipango na Maendeleo, Bi. Pendo Lauwo, kwa ajili ya shughuli za kikazi za kila siku za Idara ya Mashamba.
Ibada hiyo pamoja na makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 28/01/2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya Dayosisi, Lushoto-Tanga. Chombo hiki cha usafiri kitasaidia katika mazingira ambayo hakuna barabara zinazofikika kwa kutumia usafiri wa gari.
Kwa upande wake, Bi. Pendo ameushukuru uongozi wa Dayosisi kwa namna unavyoendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa Watumishi wake kwa kuwapatia vitendea kazi. Aidha, ameonesha imani kuwa jambo hilo halitaishia katika Idara ya Mashamba pekee, bali pia kwa idara nyingine zitakazokumbwa na changamoto ya vitendea kazi.
Pikipiki hiyo itatumika katika utekelezaji wa shughuli za kikazi za kila siku za Idara hiyo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha ufanisi wa kazi.
Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii
INSTAGRAM - / elctned
FACEBOOK ACCOUNT North Eastern Diocese
FACEBOOK PAGE - ELCT-North Eastern Diocese
YOUTUBE - / KKKT DKMS Online TV
KWA MAONI NA USHAURI:
Simu: +255 743 399 798

