
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt Msafiri Joseph Mbilu amewataka Wachungaji na Mashemasi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, kuja na mpango mkakati wa kutoa Elimu ya Kikristo mashuleni ili kuwafanya wanafuzi wamjue Mungu ili wawe na amani na ndipo mema yatakapowajia.
Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 2/3/2023 katika Ukumbi wa mikutano wa Benjamin William Mkapa Auditorium uliopo katika taasisi ya Elimu ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) Magamba Lushoto . katika kikao maalum kilicho wakutanisha Wachungaji na Mashemasi wa KKKT-DKMs. Sambamba na hilo Askofu Dkt Mbilu aliwatambulisha wawezeshaji wa neno la Mungu na kati yao kuna Mjumbe wa Kamati ya Harambee inayopangwa kufanyika Jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo Askofu Askofu Dkt. Mbilu ameendelee kuwahimiza na kuwakumbusha Wachungaji na Mashemasi kuendelea kuhamasisha washarika na wadau wengini wa maendeleo kuchangia deni la Dayosisi ambapo siku zinavyozidi kuendelea kunagundulika madeni mengine yaliyotokana na kilichokua Chuo cha Sebastian Kolowa Memorial University (SEKOMU).

