Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju, amewapongeza na kuwashukuru wachungaji na mashemasi wanawake wa KKKT-Dayosisi ya kaskazini mashariki kwa huduma nzuri wanayofanya ndani ya Dayosisi,sharika na vituo mbalimbali walivyopangiwa.

Pongezi hizo amezitoa leo tarehe 10/03/2022 kwenye ufunguzi wa mkutano Mkuu wa nne wa Wachungaji Wanawake na Mashemasi wa KKKT-Dayosisi ya kaskazini mashariki katika ukumbi wa mikutano Utondolo.

Amewashauri kuendelea kutumia fursa zilizopo katika Kanisa na jamii kwa ujumla ili kuinuana kiuchumi na kuwa wamoja,ameongeza kuwa Dayosisi inathamini huduma yao hivyo wasirudi nyuma wafanye kazi kwa bidii na kupendana ili kundi liendee kupata nguvu na kufika mbali zaidi.

Hata hivyo amewakumbusha kuwa mwaka 2022 ni mwaka wa Wanawake hivyo wahakikishe Wachungaji Wanawake wanaweka alama katika mission kubwa ya Mungu iliyowekwa mikononi mwao.

Akimuwakilisha Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu kwenye ufunguzi huo amewashukuru  kwa mwaliko wa ufunguzi wa mkutano na kuwatakkia mkutano mwema wenye majadiliano mema yenye tija kwa Kanisa na jamii kwa ujumla.