Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt Msafiri Joseph Mbilu amewapongeza vijana wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kipekee vijana wa Kanisa Kuu Lushoto kwa kazi kubwa na nzuri waliyo ifanya kwa njia ya nyimbo na walio ongoza Ibada
pongezi hizo amezitoa leo tarehe 20/02/2022 kwenye Ibada ya sikukuu ya Vijana huku akimpongeza mratibu wa Vijana na ukwata wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Alice Kopwe kwa maandalizi mazuri yanayoondelea kuelekea tamasha la Vijana na Askofu litakalo fanyika tarehe 25-27/02/2022.