Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMS) imefanya Mkutano Mkuu wa 3 baada ya miaka 125 ya Injili ulioanza tarehe 25-26/11/2020  ikumbukwe mkutano huu ulikuwa na ajenda kuu moja ya Uchaguzi wa Askofu  mpya wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na viongozi wengine.

 Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati maalumu ya kuratibu shughuli za mkutano mkuu wa uchaguzi wa Askofu ni Askofu Mstaafu Dkt. Paulo Akyoo toka KKKT Dayosisi ya Meru ambaye baada ya uchaguzi alimtangaza Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu aliye chaguliwa na Wajumbe wa mkutano Mkuu kuwa Askofu mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kupata kura 194  sawa na 89.4% .

 Askofu Mteule alimteua Mch Michael Mlondakweli Kanju ambaye alithibitishwa na mkutano Mkuu kwa kura ya Siri na kufanikiwa kupata kura 170 Kati ya 210 sawa na 80.9%.Kura hizo ni zaidi ya 2/3 ambalo ni hitaji la kikatiba.Aidha Mkutano Mkuu ulichaguwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki baada ya kupatikana kwa Halmashauri kuu hiyo ilitimiza wajibu wake wa Kikatiba wa kuchaguwa  Wakuu wa Majimbo na kuwaleta mbele ya Mkutano mkuu.

  Wachungaji wafuatao wamechaguliwa kuongoza Majimbo yafuatayo;

Mkuu wa Jimbo Mteule Mch. Anderson Kipande Jimbo La Kaskazini.

Mkuu wa Jimbo Mteule Mch.  Isai A. Mweta Jimbo la Kusini.

Mkuu wa Jimbo Mteule Mch. Thadeus A. Ketto  Jimbo la Pwani: 

Mkuu wa Jimbo Mteule Mch. Frank Mntangi Jimbo la Tambarare.