Rais wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (LWF) Askofu Henrik Stubkjær ameungana na Watanzania katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa Hemophilia Duniani ambapo jamii imeaswa  kupima mara kwa mara ili kuweza kujua hali ya Afya zao na kuchukua hatua mapema.

 Askofu Dkt. Fredrick Shoo akimwakilisha Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Alex Malasusa ameahidi kuendeleza ushirikiano hususan katika kuendelea na kukuza sekta ya Afya na Elimu.

Aidha amesema KKKT kupokea ujumbe unaongozwa na Rais wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani Askofu Henrik Stubkjær ni heshima kubwa katika kuendeleza na kuimarisha uhusiano uliopo.

 Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Daktari Bingwa wa magonjwa ya Watoto na mbobezi wa magonjwa ya damu na saratani za Watoto kutoka Hospitali KCMC, Ester Majaliwa amesema ni muhimu wazazi kuondoa hofu juu ya ugojwa huo.

Fatuma Malema ni mzazi mwenye mtoto anayepokea matibabu ya ugojwa huo na kusema mwanae aligundulika na ugonjwa huo mwaka 2022 na sasa anaendelea na matibabu na kutoa wito kwa wazazi wengine kuwahi Hospitali pale wanapogundua tofauti za kiafya kwa watoto wao.

 Hemophilia husababishwa na mabadiliko, katika moja ya jeni, ambayo hutoa maagizo ya kutengeneza protini za sababu ya kuganda zinazohitajika kuunda kuganda kwa damu. Kwa kawaida mwili hukusanya chembechembe za damu ili kutengeneza donge la damu ili kusitisha damu wakati mtu anavuja damu na hivyo kupelekea Hospital ya KCMC kuanzisha kitengo maalumu cha kuhudumia wagonjwa hao tangu mwaka 2020 na hadi sasa hospitali hiyo imewahudumia wagonjwa 26.