Print

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju amewashukuru Washarika wa Makorora na kipekee wana Dayosisi kwa ujumla kwa jinsi wanavyoendelea kuuombea uongozi na Dayosisi.

Shukrani hizo amezitoa leo tarehe 13/03/2022 kwenye Ibada ya Jumapili katika Usharika wa Makorora Jimbo la Pwani na kuongeza kuwa kwa nyakati tofauti uongozi umekuwa ukitoa taarifa juu ya madeni mbalimbali yanayo ikabili Dayosisi na Washarika wamekuwa wakijitoa kwa michango ili kukabiliana na madeni hayo hivyo kujitoa kwa Washarika ni jambo  linalo tia moyo  na kuupa nguvu uongozi kuamini kuwa madeni hayo yatakwisha.

Hata hivyo ametanabaisha kuwa uongozi unapokea maoni mbalimbali kwa watu wenye mawazo chanya yatakayo saidia kuivusha Dayosisi katika kipindi hiki kigumu.

Msaidizi wa Askofu, Mch. Michael Kanju amekuwa na ziara ya kikazi katika Jimbo la Pwani linalo ongozwa na Mch. Thadeus A. Ketto na amehitimisha ziara yake leo katika Usharika wa Makorora unao ongozwa na Mch. Peter Bendera.