Print

Mkuu wa KKKT Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo, amefungua warsha ya mafunzo ya Uongozi kwa Maaskofu wa KKKT na wasaidizi wa maaskofu ambapo masomo yaliyofundishwa katika warsha hiyo ni pamoja na, umoja wa Kanisa, uongozi Shirikishi, itifaki pamoja na mbinu za uongozi bora.Washiriki wa warsha hiyo walikabidhiwa vyeti rasmi vya kuhudhuria mafunzo hayo.



Warsha hiyo iliyofanyika hivi karibuni ilifanyia katika kituo cha mikutano cha SUN RETREAT CENTER kilichopo Marangu kinachomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini. Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu pamoja na msaidizi wake Mch. Michael Mlondakweli Kanju wameshiriki katika warsha hiyo.

Washiriki wakijifunza juu ya mawasiliano yenye ufanisi na namna bora ya kuunda mtandao wa mawasiliano baina ya watumishi wa ngazi zote.

Hits: 12259