
Watumishi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki wametembelea hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro pamoja na kufanya Uinjilishaji KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati Usharika wa Engarenarok.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt Msafiri Joseph Mbilu ameitaka jamii kwa ujumla kutunza mazingira kwa kutokukata miti hovyo na kulinda uumbaji wa Mungu.

Ameyasema hayo leo tarehe 12/03/2023 katika Ibada ya Jumapili iliyofanyika KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Engarenarok ambapo amesema kuwa utunzaji wa mazingira utaendelea kulinufaisha Taifa katika sekta ya Utalii kupitia vivutio mbalimbali vya utalii kama vile Hifadhi Ngorongoro.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mwl. Julius Samwel Madiga na watumishi wa Ofisi Kuu ya KKKT-DKMs na wa vituo walioambatana na Askofu Dkt Mbilu katika ziara ya mafunzo pamoja na Uinjilishaji kupitia uimbaji.

Aidha mbali na Ibada hiyo,watumishi wa Ofisi Kuu na Vituo walipata nafasi ya kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo ziwa Duluti na Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na kujionea faida za utunzaji wa mazingira.
