Print

Mahusino mema ni jambo zuri na la kupendaza katika jamii yoyote duniani ikiwemo serikali,taasisi hata kwenye mikusanyiko ya jamii fulani. Haya siyo tu mahusiano ya ndugu bali hata ya watu wanaokuzunguka,na hii inasadifu yanayotokea KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  kwa kutembelewa na kiongozi wa serikali ya Ujerumani na huyu siye mwingine bali ni Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini Tanzania Dkt Kathrin Steinbrenner ambaye alipokelewa na mwenyeji wake Askofu  Dkt. Msafiri Joseph Mbilu .

Ujio huu wa Naibu Balozi wa Ujerumani katika Dayosisi yetu umepokelewa kwa furaha na viongozi mbalimbali akiwemo Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki   Dkt Msafiri Joseph Mbilu ambapo Dkt  Steinbrenner anataka kujua japo kwa uchache uhusiano uliopo kati ya Ujerumani na KKKT-DKMs kwa Ujumla ambapo Askofu Dkt. Msafiri  Mbilu anaelezea historia ya kuvutia na kusisimua kuhusu Kanisa na uhusiano uliopo ambapo Askofu Dkt. Mbilu alimwelezea  mahusiano yaliyopo kati ya KKKT-DKMs na Ujerumani hususani katika suala zima lakuleta neno la Mungu, maelezo yalimfurahisha Dkt  Steinbrenner na kuahidi kuendelea kuimarisha mahusiano yaliyopo.

Baada ya kusimuliwa mahusiano hayo yaliyopo kati ya KKKT-DKMs na Ujerumani hatimaye Dkt  Steinbrenner alipata nafasi ya  kutembelea kituo cha polisi Lushoto na kujionea historia ndefu ya muda mrefu kuhusu kituo hicho cha polisi ambacho ndicho kituo cha kwanza cha polisi kuwepo enzi hizo za Tanganyika yaani toka enzi ya ukoloni pamoja na kutembelea Chuo cha uongozi wa Mahakama Wilaya ya Lushoto IJA ambapo napo akaelezwa mambo mbalimbali.

Pia alipata nafasi yakufika katika Hospitali iliyo na historia nzuri na Ujerumani ambayo inamilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Hospitali ya Bumbuli ambapo mbali na wenyeji kufurahia ujio huo lakini wakapata wasaa wa kumuonyesha na kumuelezea mambo mbalimbali  mgeni huyo wa heshima katika hospitali hiyo ikiwemo changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo  ikiwemo uhaba wa vitendea kazi kama Ambulance, X-ray Mashine pamoja na Ukarabati wa Wodi ya wanawake.

Dkt  Steinbrenner mara baada ya kusikia changamoto hizo alitoa ahadi ya kujaribu kutafuta washirika ambao watakuwa na uhusiano wa karibu na Hospitali hiyo ili wakati mwingine changamoto ndogo ndogo ziweze kutatuliwa.Pamoja na hayo Dkt  Steinbrenner alipata fursa ya kutembelea  Chuo cha BUCOHAS ambacho kinamilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  na hapo pia alielezwa kuhusiana na mfumo wa elimu pamoja na mafanikio ambayo yamepatikana ndani ya Chuo hicho.

Dkt  Steinbrenner alihitimisha ziara yake katika kiwanda cha uchapishaji cha Vuga Press Publishing House kilichopo Soni Wilayani Lushoto ambapo mbali na kupewa historia ya kiwanda hicho na Meneja wa kiwanda hicho Mch. Moses Shemweta lakini ameweza kujionea  mashine za uchapishaji ambazo zilitumika enzi hizo na wajerumani, nyingine zikiwa zinafanya kazi na nyingine zikiwa hazifanyi kazi huku akiahidi kuyaelezea hayo kwa wajerumani wenzake ili kuendelea kuilinda na kuitunza historia nzuri iliyoachwa na wajerumani hususani katika Kanisa.

 

Hits: 13401