Print
 
Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju amefungua kikao cha wadau wa kutengeneza mtaala wa Diakonia, Ustawi wa Jamii na Speech ideology kilichofanyika katika ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopa katika chuo cha Kolowa Technical Training Institute ( KOTETI) Magamba leo tarehe 3/02/2023.
Mtaala huu unategemewa kuwa moja wapo ya kozi zitakazo tolewa katika taasisi ya Elimu KOTETI. Mch. Kanju aliongeza kuwa Dayosisi  imebobea katika kutoa huduma za kijamii za Kidiakonia kwa kuwa na vituo vingi ambavyo vinawafikia watu wenye mahitaji maalum.
Nae Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Lushoto Bi. Glory Mdemu ameishukuru Ofisi ya Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kuja na wazo la kuanzisha Mtaala ambao unaakisi uhalisia ambao upo kwenye jamii hivyo Serikali kupitia Ofisi ya Mkurugenzi ipo tayari kupokea wataalam watakaopata elimu hiyo kupitia Taasisi ya KOTETI.
Hits: 11843