Print

Nikasikia sauti  kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho wapate kupumzika baada ya taabuzao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nayo.

Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Godfrey Tahona Walalaze amesema kuwa wanadamu wanaogopa sana kitu wasicho kijua na hasa wasichoweza kukidhibiti na kifo nimojawapo ya kitu ambacho kipekee  wanadamu wote hawakijua kwani wanafikiri juu ya kifo  wanazungumza juu ya kifo lakini hakuna ajuaye saa wala dakika na wakati wa kukutana na kifo na kwa sababu hiyo kifo kimeendelea kuleta hofu kwenye maisha ya wanadamu .

 

Mch Godfrey  Walalaze ameyasema hayo leo tarehe 24/01/2022 kwenye  Ibada ya mazishi ya Bibi, Mary Shebila katika Kijiji cha Baghai-Vuga akihubiri  neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 14: 13.

Ameongeza kuwa ni heri kufa katika Bwana yaani Bwana wetu Yesu Kristo  kwani kifo chako  kitakuwa heri na pumziko liko mbele yako baada ya maisha haya.kwa kila  anaye mwamini ana heri maana yeye alishinda mauti kwa ajili yetu na kwakila anaye weka maisha yake dhamana mikononi mwake Yesu hata akifa kifo cha mwili anauhakika wa kuuridhi uzima wa milele maana ule utu wa ndani unauhakika wa kukutana na yeye ambaye ameshinda mauti na kuzimu.

Bibi Mary Shebila alizaliwa tarehe 12/08/1938  na kuitwa mbinguni asubuhi ya tarehe 19/01/2022, alifunga ndoa na   Mzee Fedrick Laban Shebila katika Usharika wa Mombo mwaka 1963, Mzee Frederick  Shebila amabaye pia ni marehemu katika uhai wake aliwahi kuitumikia KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Masharika katika nafasi ya Katibu Mkuu.

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unaendelea kutoa pole kwa,familia ya marehemu   ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.

 

Hits: 14844