Print

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amekutana na kufanya mazungumzo na Mratibu wa Mawasiliano wa KKKT, ndugu Erick Adolph ambae ametembelea Makao Makuu ya KKKT-DKMs leo tarehe 19 Novemba, 2021.

Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akizungumza na Mratibu wa Mawasiliano wa KKKT, ndugu Erick Adolph

Lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kuushirikisha uongozi juu ya umuhimu wa kuwa na Mratibu wa Mawasiliano na Habari wa Dayosisi, wazo ambalo uongozi wa KKKT-DKMs umelichukuwa na kuahidi kulifanyia kazi.

Kwa upande mwingine Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amemuahidi mratibu huyo ushirikiano wakutosha kwani ni mojawapo ya mipango ya Dayosisi kuhakikisha wanadayosisi wanapata taarifa sahihi juu ya mambo yanayofanyika katika Dayosisi yao na Kanisa kwa ujumla.

Hits: 14896