Print

“……Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”

Leo tarehe 07/11/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa Usharika wa Kana, Jimbo la Pwani, ambapo vijana wapatao 33 walibarikiwa na mmoja kati yao alibatizwa.

 

Katika Ibada hiyo,Liturgia iliongozwa na Mkuu wa Jimbo la Pwani Mch. Thadeus A. Ketto na msaidizi wa Askofu, KKKT-DKMs Mch. Michael Mlondakweli Kanju  alihubiri neno la Mungu.

Ibada ilihudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti,Mashemasi, Kwaya,Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Kana.

Vijana waliopata kipaimara walitoa kiasi cha Tsh 120,000/= kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki katika masuala ya elimu.

Aidha vijana hao katika risala yao wamewashukuru  watumishi wa usharika  wa Kna kwa kuwatufundisha neno la Mungu kwa usahihi wake, katekisimo ndogo ya Daktari Martin Luther, masomo mbalimbali yanayohusu imani  ya Kikristo.

Mbali na hayo wamemshukuru Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu kwa kazi mbalimbali za huduma,maendeleo na Uinjilisti katika Dayosisi kama vile mpango wa kuendeleza Mission ya Mungu kupitia Radion ya Dayosisi Utume Fm Radio,mfuko wa maendeleo wa Dayosisi Hospitali za Dayosisi vituo vyote pamoja na kazi mbalimbali zinazo endelea katika Dayosisi.

Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs Mch. Michael Mlondakweli, ambaye alimwakilisha  Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu katika Ibada hiyo, katika itikio la risala ya vijana hao aliwashukuru  vijana hao kwa risala yao nzuri kwa kutambua kazi nzuri inayoendelea kufanyika katika Dayosisi.

Hits: 17218