Print

 

 

TANZIA

 

"Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza  yamekwisha kupita " UFUNUO 21:4.

 Kaimu Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya Uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Baba Mzazi wa  Mch. Lemmy Baruti, Mzee Tamilwai Augustino Baruti kilichotokea usiku wa tarehe 31/10/2021 katika hospitali ya Wilaya ya Pangani.

 Taratibu za mazishi zinaendelea na mtajulishwa.

 Uongozi unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.

 

...........                ................                    .................                      .....................

 

Hits: 15239