Print

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Inatangaza Nafasi  moja ya Kazi ya KATIBU WA AFYA WA DAYOSISI.

MAJUKUMU YA KAZI INAYOOMBWA NI PAMOJA NA:

  1. Kutayarisha Mipango na Makisio ya fedha za shughuli zinazohusiana na Afya
  2. Kutayarisha Taarifa za Shughuli za uendeshaji na Utekelezaji za Mwezi,Robo mwaka na Mwaka mzima.
  3. Kusimamia matumizi ya Fedha na ununuzi wa Vifaa kama ilivyo katika miongozo ya fedha na ununuzi.
  4. Kusimamia na kutathimini utendaji wa kazi wa Watumishi kulingana na taratibu zilizokubalika.
  5. Kuandaa Mipango ya Usafiri kwa Wagonjwa
  6. Kutoa ushauri wa Kiutawala katika masuala ya kila siku kuhusu utekelezaji wa shughuli za Afya.
  7. Kufundisha watumishi utunzaji wa rasilimali za Afya (Watumishi,fedha,vifaa na muda)
  8. Kusimamia na kutathimini uendeshaji shughuli za Afya.
  9. Kuitisha Vikao mbalimbali pamoja na kuandika mihutsari ya Vikao hivyo vya kiutendaji.

SIFA ZA MUOMBAJI

  1. Mwenye Elimu ya Kidato cha 4 au 6 na aliehitimu mafunzo ya shahada ya Kwanza ya Menejimenti ya Afya (Health System Management katika Chuo kinachotambulika na Serikali ya Tanzania.
  2. Awe Mtanzania na mwenye umri usiozidi miaka 45.
  3. Uzoefu wa Kazi sio chini ya Miaka 2.
  4. Maombi yote yaambatanishwe na Nakala ya Vyeti vya taaluma na vya Kidato cha 4 au cha 6 pamoja na cheti cha kuzaliwa.
  5. Waombaji waambatanishe maelezo yao binafsi yaliojitosheleza na yenye anuani zao na namba zote za simu, Na picha 2 za passport za hivi karibuni ya muombaji

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 06/11/2021 Saa tisa na nusu (09:30) Alasiri, Maombi yote yatumwe kwa Ofisi ya Katibu Mkuu-KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki S.L.P 10 LUSHOTO Barua Pepe This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Hits: 15409