Print

 

Leo tarehe 28 Januari kumefanyika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Idara ya Jinsia na Watoto KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Ufunguzi huu ulifanywa na Askofu Mteule, Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu .Mkutano huu unafanyikia katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU). Katika hotuba yake ya Ufunguzi Askofu Mteule alitoa wito kwa Idara hii kufikiri juu ya miradi mbalimbali.Aidha Askofu Mteule amewahakikishia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Idara ya Jinsia na Watoto kuwa ofisi ya Dayosisi anayoiongoza iko tayari kushirikiana na idara na kushauri juu ya mawazo yoyote ya kuanzisha miradi.

 

Askofu Mteule Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Idara ya Jinsia na Watoto.

Mratibu wa Idara ya Jinsia na Watoto KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki , Mch. Happyness Diu akitoa taarifa fupi ya Mkutano na kumkaribisha mgeni rasmi kufanya ufunguzi wa mkutano.

Mratibu wa Idara, Mch. Happyness Diu ameeleza kuwa, mkutano huu unaendelea hadi tarehe. 30 Januari 2021 na unatarajiwa kuwa na uchaguzi wa viongozi wa Idara katika ngazi ya Dayosisi kwa miaka minne ijayo. Pamoja na hayo ameeleza kuwa kutakuwepo  na uwasilishwaji wa mada mbalimbali.

Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Idara ya Jinsia na Watoto wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa mkutano mkuu  wa Idara.

Mkurugenzi wa Huduma za Jamii Mch. Joyce Kibanga mwenye kola kushoto pamoja na  Mratibu wa Idara ya Jinsia na Watoto Mch. Happyness Diu mwenye kola kulia katika maandamano kuelekea ufunguzi wa mkutano wa Idara.

 

Hits: 17953