Print

Askofu Mteule Mch. Dr. Msafiri Mbilu na viongozi wengine wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU wamemtembelea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa .

 Ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi mpya wa  KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambao ndio wamiliki wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) ukamilishe mahitaji ambayo yataiwezesha Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kukiruhusu chuo hicho kuendelea na udahili.

Mhe. Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, Januari 16, 2021 wakati alipokutana na Askofu Mteule Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ambaye aliambatana na  viongozi wengine wa Dayosisi. Kikao  kimefanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa Dododoma.

Dean Mteule  wa KKKT-DKMS,Mch. Michael Kanju akisalimiana na  WAZIRI MKUU waTanzania,Mhe.Kassim Majaliwa 

Kaimu Katibu Mkuu wa KKKT-DKMS  Mch. Godfrey Walalaze akisalimiana na WAZIRI MKUU waTanzania, Mhe.Kassim Majaliwa 

 Mkuu wa Jimbo Mteule wa jimbo la  Pwani Mch. Thadeus Ketto akisalimiana na WAZIRI MKUU waTanzania, Mhe.Kassim Majaliwa

Mkuu wa Jimbo Mteule wa jimbo la  Kaskazini Mch.Anderson Kipande,  akisalimiana na WAZIRI MKUU waTanzania,Mhe. Kassim Majaliwa

 Mkuu wa Jimbo Mteule wa jimbo la  Tambarare Mch. Frank Mtangi, akisalimiana na WAZIRI MKUU waTanzania, Mhe. Kassim Majaliwa

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SEKOMU  Prof. Vincent Kihiyo, akisalimiana na WAZIRI MKUU wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa

 Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango,Fedha na Utawala Prof. Joseph Mbatia akisalimiana na  WAZIRI MKUU wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa

 

Mhe. Kassim Majaliwa, ametumia fulsa hiyo kuwashukuru viongozi wa Dini Nchini kwa mchango mkubwa kwa Taifa ambapo amesema "Viongozi wa Dini ni watu muhimu sana, Inchi imetulia na ina amani , hivyo kuwa kimbilio kwa waliokosa amani makwao"

Hits: 19487