Print
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameendelea na ziara yake ya kutembelea Jimbo la Pwani na Sharika zake ambapo tarehe 20/04/2024 ametembelea Usharika Mteule wa Lugongo na kuongoza Ibada ya Shukrani.
Akihubiri katika Ibada hiyo Askofu Dkt. Mbilu ameendelea kuzipongeza kwaya katika uimbaji mzuri na kutoa wito kwa waimbaji kuendelea kuzingatia uimbaji ulio sahihi na kufuata note badala ya kurekodi midundo na kucheza muda mrefu na kushindwa kufanya Uinjilisti sahihi kupitia uimbaji.
Askofu Dkt. Mbilu amewakumbusha Wanadayosisi ya Kaskazini Mashariki na Wakristo kwa ujumla kuendelea kutafuta kumjua Mungu kwa bidii zaidi ili kuwa na Amani na watu wote ili kupata mafanikio katika maisha ya kila siku.
Pamoja na hayo Askofu Dkt. Mbilu amewasihi wana KKKT-DKMs kuendelea kuwa wamoja na kujitoa katika kazi za pamoja ikiwemo maendeleo ya Dayosisi huku akiwataka kuendelea kujitoa kwa moyo na kushiriki kwa pamoja katika kumaliza Deni la Dayosisi.
Huu ni mwendelezo wa ziara ya kikazi ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ambapo katika siku hii ya pili ya ziara yake katika Jimbo la Pwani amefungua kikao cha wazee wa Kanisa katika Usharika wa Maramba.
Askofu Dkt. Mbilu ameambatana na Msaidizi wa Askofu Mch.Michael Mlondakweli Kanju,Mkuu wa Jimbo la Pwani Mch.Frank Mtangi na aliyekua Kaimu Mkuu wa Jimbo la Pwani Mchungaji mstaafu Mch. Emmanuel Mtoi.
Siku ya kesho 21 April 2024 ataongoza Ibada ya JUMAPILI katika Usharika wa Maramba.
 
 
Hits: 764